Header Ads Widget

TMFD YAKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO KUWEKA MIKAKATI YA UVUVI ENDELEVU

 




Mwandishi wetu_Dar es Salaam


Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries  Development (TMFD) limekutana na wadau wa kimaendeleo na kufanya majadiliano mafupi ya namna ya kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu Nchini.


Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amekutana na wadau hao Jijini Dar es salaam na kuitambulisha TMF na kazi zake kwenye eneo la uvuvi na vyombo vya habari.


Soko amekutana na Naibu  Balozi wa Norway Nchini Tanzania Bwana Kjetil Schie na kujadili fursa za kutumia vyombo vya habari kwenye kuhamasisha uvuvi endelevu.


Bwana Schie amesema kuwa anafurahishwa sana na uwepo wa TMFD kwenye eneo la uvuvi kwa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuhamasisha  uvuvi endelevu kwa kutumia vyombo vya habari



Pia mkurugenzi wa TMF mekutana na kufanya mazungumzo na  Mwakilishi Mkazi wa shirika la maendeleo la kimataifa la JICA Bibi Murao Akari juu ya umuhimu wa kuendeleza uvuvi kwa kutumia njia bora..


Bwana Soko amesema kuwa kwa sasa TMFD inajikita kwenye kupanua uwigo wa wadau ili kufanya kazi kwa pamoja kwa nia ya kuendeleza uvuvi endelevu Nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI