Header Ads Widget

TAKUKURU YABAINI MAPUNGUFU MRADI WA ICU KISARAWE.

 


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Pwani imebaini mapungufu ya vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 29.4 kutokuwepo kwenye mradi wa Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) la Wilaya ya Kisarawe lenye thamani ya milioni 300.


Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Pwani Christopher Myava alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuelezea utendaji kazi kipindi cha miezi mitatu Januari hadi Machi mwaka huu.


Myava alisema kuwa waligundua kuwa vifaa hivyo vilinunuliwa kwa bei kubwa tofauti na ile ya soko na havikutumika kwenye ujenzi na havikuwepo kwenye eneo la ujenzi.


"Kufuatia mapungufu hayo tuliyobaini uchunguzi unaendelea na ukikamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa wahusika,"alisema Myava.


Alisema kuwa mradi huo ni moja ya miradi mitatu iliyokutwa na mapungufu baada ya kufanyiwa ufuatiliaji yenye thamani ya bilioni 4.9 kati ya 40 iliyochunguzwa yenye thamani ya shilingi bilioni 9.6 katika kipindi hicho.


"Kwenye mradi wa pili wa maendeleo ya jamii ni kutokuwepo kwa miradi iliyoombewa mikopo na kupitishwa na kamati ya fedha ambapo kikundi cha Twaweza kata ya Tangini Halmashauri ya Mji Kibaha kilipewa mkopo wa milioni 21kwa ajili ununuzi wa nafaka badala yake walianzisha duka la nyama na hawajarejesha mkopo tangu wakope mwaka 2022,"alisema Myava.


Alibainisha kuwa fedha hizo zilizokopeshwa ni sehemu ya fedha zinatokana na aslimia 10 ya mapato ya Halmaahauri ya Mji Kibaha ambapo ni bilioni 4.5 na makundi maalumu yanayokopeshwa ni wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. 


Aidha alisema kuwa Mradi wa tatu wa ujenzi shule ya msingi Madege Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ulikutwa na mapungufu ya kukosekana kwa ubora wa sakafu ya madarasa mawili na ofisi ya mwalimu na uwepo wa mipasuko kati ya fremu za milango na kuta kwenye mradi wenye thamani ya shilingi milioni 112.5.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI