Header Ads Widget

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU KATIKA SEKTA YA ELIMU,NI FURSA KWA WATANZANIA KUPATA ELIMU BORA.

 




Na,Jusline Marco;Arusha



Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe.John Danielson Palangyo amesema kuwa Serikali ya Awamu ya sita inaendelea kuboresha sekta ya elimu nchini kwa kujenga miundombinu bora na rafiki wa kujifunzana kufundishia.



Mhe.Palangya ameyasema hayo katika maafali ya walimu maalum kwenye ngazi ya astashahada na cheti katika Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi kilichopo Wilayani Arumeru.



Ameongeza kuwa serikali inadhamiria kuhakikisha kwamba watanzania wote wanapata elimu kwa kuzingatia haki ya kila mmoja kuanzia vyuo vya ualimu mahitaji maalum,shule za sekondari mahitaji maalum,shule za msingi mahitaji maalum lengo ni kuhakikisha wale wote wenye mahitaji maalum hawakosi fursa za kusoma.



Katika kukabiliana na changamoto ya ajira kwa walimu wa elimu maalum,ameahidi kushirikiana na TAMISEMI kuangalia namna bora ya kuwatambua walimu wa elimu maalumu wanaohitimu nchini wanaorodheshwa kuhakikisha wanapangiwa katika shule zenye uhitaji kwani wahidaji wa elimu maaljm nchini ni wengi.



Aidha amewataka wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata kuhakikisha wenye ujitaji maalum wanapata elimu kwani lengo la serikali mi kuhakikisha kila moja anapata elimu iliyo bora.



Kwa upande wa mmomonyoko wa maadili Mhe.Palangyo amesema kuwa serikali ipo kwenye operesheni kuhakikisha kwamba inatokomeza viashiria vyovyote vile vinavyoshiria kuwepo vitendo vya uharibifu wa maadili.




Naye Mkuu wa Chuo cha Ualimu Elimu Maalum Patandi,Lucian Segesela amesema kuwa huduma ya kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum bado haijawafikia walengwa wengi kwasababu ya kukosa wataalam hivyo kama chuo wamejipanga kuwaandaa walimu wa kuwasaidia watoto  mashuleni na siyo mitaani wala kwenye kada nyingine.



Vilevile ameeleza kuwa ni vyema kwa sasa serikali ikaweka mipango ya namna ya kuwaandaa wataalam wa elimu maalum wa sekta nyingine ikiwemo sekta ya Afya,Sheria pamoja na usalama barabarani kujifunza ukalimani wa lugha ya alama kwani sekta hizo ndizo zinawalaji wengi wa huduma ya elimu maalum.



Ameiomba wizara ya elimu kuruhudu vyuo vya elimu maalum kutoa kozi za muda mfupi kwa watu wa sekta nyingine ili kuwawezesha kupata umahiri wa kuwahudumia wateja wao wanapowafikia.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI