Na HADIJA OMARY _LINDI....
Yusra Hassan Ally mwanafunzi wa darasa la pili kutoka kata ya Nyegedi, halmashauri ya Mtama, mkoani Lindi, amejinyonga hadi kufa kwa kutumia nguo ambapo mpaka sasa sababu ya kujinyonga kwake haijafaamika
Kwa mujibu wa Taarifa ya jeshi la polisi Mkoani Lindi iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Afisa Mnadhimu wa jeshi hilo Kamishna msaidizi wa Polisi Alhaji Kabaleke, inasema tukio hilo limetokea siku ya tarehe 17 majira ya saa nane mchana katika kata ya nyengedi halmashauri ya mtama Mkoani Lindi.
Alhaji Kabaleke alisema kuwa, binti huyo mwenye umri wa miaka 11 alikuwa akiishi na bibi yake, ambapo siku hiyo ya tarehe 17 alishindwa kwenda shule kwa kisingizio kuwa anaumwa, ambapo aliweza kufanya kazi za nyumbani ikiwemo kufua nguo zake .
Alisema baada ya kumaliza kazi hizo binti huyo alionekana akichukua nguo na ndoo na kuamua kujitundika kwenye mti na kupoteza maisha .
"Baada ya kukagua eneo la tukio na kuwahoji watu waliokuwepo maeneo yale sambamba na kufanya uchunguzi kwa mwili wa marehemu huyo jeshi la polisi lilibaini kwamba binti huyo ni kweli sababu ya kifo chake ni kujinyonga"
" Alisema pamoja na kuwahoji majirani wa karibu na familia ya binti huyo lakini hatukubaini kwamba binti huyo kuwa alikuwa akipata mateso ya aina yoyote kutoka kwa Bibi yake aliekuwa anaishi naye " alifafanua kabaleke
Hata hivyo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi A bwana Omari Baisa akizungumza na Matuko Daima alisema kuwa, marehemu Yusra kwa muda mrefu alikuwa akiishi na Babu yake mzaa Baba kutokana na wazazi wake kuishi nje ya kijiji hiko
Alisema akiwa huko alishindwa kupata mahitaji yake muhimu kama sabuni na vitu vingine kwa ajili ya shuleni pia inadaiwa alishikwa na homa huku familia yake (babu) akishindwa kumpeleka katika kituo cha Afya kwasababu ya kukosa fedha.
Baisa alisema kuwa, kwa kuona adha hiyo Yusra aliamua kwenda kwa bibi yake mzaa mama anaeishi katika kijiji cha nyengeni na kumweleza yanayo msibu.
" alipofika bibi yake alimpokea ambapo siku iliyofuata walienda shambani kukata mpunga walipofika nyumbani waliuanika ambapo bibi yake alimuomba Yusra aangalizie mpunga usiliwe na kuku wakati yeye anakwenda sokoni kutafuta kitoweo baada ya yule bibi kutoka yusra ndipo akachukua maamuzi ya kuchukua nguo ( kitenge pamoja na ndoo na kuzunguka nyuma ya nyumba na kujinyonga"
0 Comments