Header Ads Widget

MRADI WA RAFIC WAWAPELEKA WANAFUNZI 29 WA DIT KENYA KUJIFUNZA

 Na Adery Masta


Mkuu wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam Prof. Preksedis Ndomba akizungumza na  WANAFUNZI 29 wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam  (DIT) wa Stashahada ya Uhandisi Umeme kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini Kenya katika Chuo cha MERU NATIONAL POLYTECHNIC kwa masomo ya mwezi mmoja.


Picha ya pamoja Uongozi wa Taasisi ya Teknolojia Dar Es Salaam DIT na WANAFUNZI 29 wa Stashahada ya Uhandisi Umeme muda mchache kabla ya safari ya kwenda  nchini Kenya katika Chuo cha MERU NATIONAL POLYTECHNIC kwa masomo ya mwezi mmoja.

......................................

WANAFUNZI 29 wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam  (DIT) wa Stashahada ya Uhandisi Umeme wamekwenda nchini Kenya katika Chuo cha MERU NATIONAL POLYTECHNIC kwa masomo ya mwezi mmoja.

Wanafunzi hao wameambatana na mwalimu wao mmoja Halima Libani. Safari hiyo ni programu ya kubadilishana wanafunzi ambapo kwa upande wa Meru wanakuja wanafunzi 30 na mwalimu mmoja. 

Programu ya kubalidishana wanafunzi inafadhiliwa na mradi wa EASTRIP unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ambao kwa DIT Kampasi ya Dar es Salaam unalenga kuanzisha Kituo cha Kikanda cha  Umahiri wa TEHAMA kitakachoitwa RAFIC.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS