Header Ads Widget

MAFISA BIASHARA JENGENI URAFIKI NA WAFANYABISHARA

 





Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma.


MAARIFA  Biashara nchini wametakiwa Kujenga urafiki wa karibu na wafanyabiashara hali itakayosaidi ukusanyaji wa mapato kuongezeka katika mikoa na Halmashauri husika .


Hayo yamesemwa jijini hapa na Mkurugenzi wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Ofisi ya TAMISEMI Conrad Milinga kwenye kikao cha Kuthibitisha Mwongozo wa Wataalam wa biashara.


Mkurugunzi huyo amesema ni wakati Sasa wa maafisa biashara kuwa na mahusiano mazuri kwa kuwa  marafiki na wafanyabiasha ili kuikuza nchi Kiuchumi. 


Aidha amesema Serikali ya awamu ya Sita imejipambanua Kufungua nchi hivyo analeta wawekezaji hivyo ni vyema wawepo watekekezaji nchi inafunguka na watendaji wawepo hivyo ndio Maana ikaanzishwa idara hii ya uwekezaji viwanda na kuanzia ngazi ya mikoa ili iendane na lengo la Rais Samia Suluhu Hassan.


Amesema Serikali ina majukumu  yake hivyo pengine bado tunaendelea na mawazo yale yale ya zamani hatujatoka sana kwenye mawazo ya ujamaa tunapiona sekta binafsi tunaitazama kwa mitazamo hasi.


Watendaji wa serika tunapoiona sekta binafsi wamekuwa wakipambana nayo wakiiona kama ni sekta shindani badala yake waione ni moja ya jitihada zinazofanywa na Serikali.


Kama wizara wameona kuna changamoto hivyo Wanaandaa Mwongozo wa kuwawezesha wafanyabiashara na wajasiriamali wanapotaka kuanzisha biashara zao wajue wanaanzia wapi na kuishia wapi .


Sangu Deogratus Katibu Tawala Msaidizi katika sekretariet mkoa wa Kigoma viwanda na uwekezaji Amesema muundo wa sehemu katika sekretariet ya mikoa sehemu ya viwanda na biashara.


Wanashukuru Serikali ya awamu ya Sita baada ya kuunganisha majukumu ya wizara ya uwekezaji viwanda na biashara na utendaji wa Serikali za Mitaa kwa kuanzisha idara hiyo ya viwanda biashara na uwekezaji ili kazi hizo ziweze kufanyika kwa wakati sahihi kwani zamani utekekezaji wa majukumu hayo yalikuwa magumu kufanyika.


Wataalamu wa biashara kuwa na mahusiano mazuri tuwe marafiki na kuahidi wanakwenda kuyafanyia kazi mafunzo yote waliopatiwa.


Semdoe Manongi Nyale kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya biashara Wizara ya uwekezaji viwanda na biashara Amesema wamekuwa na semina iliyowakutanisha  makatibu wasaidizi na makatibu Tawala wasaidizi wa mikoa kupitisha juu ya Nini wanataka kufanya katika wizara  na utekekezaji wa majukumu yao.


" Sasa hivi Serikali yetuj imekuwa ikihamasisha Mazingira Bora ya kufanya biashara na uwekezaji wizara inatengeneza mwongozo utakao rahisisha utendaji kazi katika ngazi za mikoa Halmashauri na Wilaya hivyo ni vyema tumeona tuwapitishi wenzetu na kuona wapi tumefukia juu ya Muongozo huu.


Amesema vitu vyote vilivyokuwa vikwazo vinakwenda kuondolewa kupitia Wizara yetu ili Watu wafanye kazi kuongea lugha moja kuanzia wizara Hadi ngazi ya chini.


Amesema katika kuboresha Mazingira ya biashara Serikali imetengeneza idara mpya chini ya wizara ya TAMISEMI katika ngazi ya mikoa na Halmashauri kitengo Cha uwekezaji viwanda na biashara  wanapitishana kwenye majukumu hayo kuelimishana na kuelewana ili utekekezaji uwe rahisi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI