Header Ads Widget

MADAKTARI WA VIUNGO BANDIA WAONGEZWE KCMC...PROF NDAKIDEMI

 


Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP


Wagonjwa ambao ni maskini wenye uhitaji wa viungo bandia wamehitajika kuhudumiwa kikamilifu na serikali badala ya kuachiwa jukumu hilo pekee ambalo linaonekana kuwaelemea.


Kadhalika kutokana na hali hiyo imeonekana kuwa mzigo mkubwa kwa kaya maskini jambo linalozidi kuwaongezea ugumu wa maisha wagonjwa hao badala ya kuwaletea faraja.


Haya yanabainishwa na mbunge wa Moshi Vijijini, Profesa Patrick Ndakidemi wakati akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya afya kuelekea bajeti ya mwaka 2023/2024. 


Aidha ameomba hosptali ya Kanda ya KCMC iongezewe madaktari na wahudumu wa sekta ya afya kwani hivi sasa kuna upungufu mkubwa wahudumu hao


"Hospitali ya Kanda ya KCMC ipo haja sasa iongezewe madaktari na wahudumu kwani waliopo kwa sasa hawaendani na hali ya uhitaji wenyewe"amesema


Hata hivyo baadhi ya wadau katika sekta ya afya akiwemo Glory Kiwelu amesema watu wenye uhitaji wa viungo bandia bado hawapati kipaumbele na hivyo jitihada ziongezwe kuwasaidia


"Huku na kwenyewe kuongezewe nguvu kama ilivyo kwa wagonjwa wengine vinginevyo tunawabebesha msalaba wasiouweza na inatakiwa serikali ilete ahueni"amesema


Judith Mmasy naye alisema watu wenye uhitaji wa viungo bandia wanatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu lakini pia viungo vipatikane kwa bei rahisi tofauti na ilivyo sasa.


"Itakuwa vyema kama sisi wenye ulemavu lakini tunaohitaji viungo tukipewa uangalizi wa kipekee na kutuwezesha kupata viungo kwa bei rahisi tofauti na sasa ikiwa hivyo tutakuwa tumejikomboa kama taifa"amesema





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI