Header Ads Widget

CHONGOLO ATOA AGIZO KWA RC IRINGA KUSIMAMIA USOGEZAJI UMEME VITONGOJI VYOTE VISIVYO NA UMEME


 KATIBU mkuu wa chama Cha Mapinduzi (CCM)Daniel Chongolo amemuagiza mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kusimamia zoezi la uingizaji umeme Katika vitongoji vyote vya mkoa huo .


Chongolo ametoa agizo hilo leo wakati akizungumza na wananchi wa  Ilambilole kata ya Kising'a Jimbo la Isimani.


Alisema kuwa umeme si anasa Kwa wananchi ni huduma ya msingi ambayo wanapaswa kupata hivyo ni lazima wananchi wote kusogezewa huduma ya umeme .


Chongolo alisema Lengo la Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha wananchi wote waliopo mijini na Vijijini wanapatiwa huduma za msingi kama umeme ,Maji ,huduma za Afya na kuwa na Miundo mbinu Bora ya barabara hivyo ni wajibu wa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kuona wanasimamia Utekelezaji wa Ilani ya CCM.


Hivyo alisema ndani ya mkoa wa Iringa ni Matumaini ya CCM kuona wananchi wote ambao vitongoji vyao havijafikiwa na umeme kupelekewa huduma hiyo .


Katika hatua nyingine Chongolo ameagiza zoezi la usogezaji huduma ya Maji Vijijini iongezewe kasi zaidi ili changamoto ya Maji Kwa maeneo yasiyo na huduma hiyo kuwa na Maji ya uhakika .


Awali wakala wa Nishati vijijini (REA) Khamis Mrope alisema kuwa ndani ya mkoa wa Iringa Kuna vitongoji 248 ambavyo hazina umeme na mpango wa REA kufikisha umeme Katika vitongoji hivyo .


Alisema Kwa wilaya ya Iringa kuna vitongoji 121 ,Kilolo vitongoji 49 na Mufindi vitongoji 78 kuwa vitongoji hivyo 248 vipo kwenye mpango wa kuingizwa umeme Mwezi   wa Saba Mwaka huu na zoezi la kutafuta mkandarasi linaendelea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI