Taarifa za kusikitisha za kushtua zilizotufilia na kuwa aliyewahi kuwa Waziri wa mambo ya Nje Bernard Kamilius Membe amefariki Dunia Katika Hospital ya Kairuki Mkoani Dar es salaam.Taarifa za awali zinadai kuwa alipata changamoto yaKifua na kupelekwa Hospitalini hapo Alfajiri Leo na wakati akipatiwa matibabu ndipo alipofariki
Taarifa kutoka ndani ya familia zinasema taa ya Membe ilizima ghafla asubuhi ya leo Ijumaa, Mei 12; Hospital ya Kairuki (HK) iliyoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam, akiwa anapatiwa matibabu, baada ya kupelekwa siku tatu zilizopita kwa changamoto ya homa na kifua.
Membe ambaye anatajwa kama Kachero mbobevu na Mwanadiplomasia nguli na Mwanansiasa makini, aliwahi kugombea nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu 2020, akipeperusha bendera ya ACT Wazalendo
Bernard Kamilius Membe, (born 9 November 1953- Died 12 May 2023) was a Tanzanian politician. He served as a Minister of Foreign Affairs of Tanzania from 2007 to 2015.He also served as a Member of Parliament for Mtama constituency from 2000 to 2015.
0 Comments