Na Mwandishi Wetu
Wataalam wa kilimo nchini wameshauriwa kuwatembelea wakulima na kutoa elimu ili kuiinua Sekta ya kilimo.
Akizungumzia juu ya teknolojia katika sekta ya kilimo nchini Mkurugenzi Mtendendaji wa Chama cha Wafanya Biashara Wenyeviwanda na Kilimo nchini (TCCIA) Nebart Mwapwele amesema wataam wa kilimo wakiwafikia zaidi wakulima nchini watawezasha kilimo chenye tija.
Amesema Serikali imeendelea kuimarisha huduma za ugani kwa kugawa pikipiki 7000 ,sekta ya kilimo imeendelea kuwa muhimili Mkuu wa kukuza uchumi nchini na kuleta maendeleo ndani ya nchi.
"Kuendelea kutumia wataalam wetu mashambani kutasababisha mkulima kuelewa namna bora ya uifadhi wa mbegu na hivyo kufanya kichocheo kikubwa katika kilimo chenye tija"amesema Mwapwele.
Amesema nchini yapo maeneo mazuri yanayo vuna mazao mengi ya kilimo kikifanyika kitaalamu na kuvuna mazao mengi .
"Mfano mzuri ni mashamba yanayolimwa Mbalali mkoani Mbeya ambapo maafisa ugani wamekuwa wakitoa elimu kwa muda mrefu nakusababisha kilimo chenye tija,"amesema Mwapwele.
Mwapwele anasema Serikali inapambanua kuwa mchango wa maafisa ugani ni kuhakikisha kwamba wanawafikishia teknolojia sahihi wakulima, wafugaji na wavuvi ili kuongeza uzalishaji na tija kwa ajili ya usalama wa chakula, kuongeza kipato na kupata mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyetu.
Hivyo hivyo kuelekea uchimi wa juu wa kati , maafisa ugani watasaidia kuwawezesha wakulima, wafugaji na wavuvi kutambua mbinu bora za kufikia masoko ya mazao yao.
0 Comments