Chama cha Wafanyabiashara Ndogondogo Mkoa wa Dar es Salaam (KAWASSO) katika kipindi cha mwaka huu wamesema kuna mwanga mpya wa fursa kupitia kwa wadau wa Banki Maendeleo kwa kuwa 2023 Benki hiyo inatarajia kuwafikia Wamachinga zaidi ya elfu tano, pamoja na makundi ya Wanawake na vijana kuwapatia Elimu ya biashara na kuwapatia mikopo yenye riba nafuu kwa wale wanaokidhi vigezo ili kuweza kuwainua kiuchumi.
Akizungumza jana Dar es Salaam Mmoja wa viongozi wa juu kupitia KAWASSO,Augustino Atanas Choga amesema kuwa Benki hiyo imeweza kuwapatia mikopo ambapo imewafikia Wamachinga 1800 kwa mwaka jana kusababisha kuinua uchumi wa kila mmoja," anasema Choga.
Amesema jumla ya wamachinga wakiume waliopata mikopo hiyo 1244 na kufurahia uchumi wao kukua baada ya kuwezeshwa.
"Sisi kama sehemu ya Uongozi huu wa Machinga tunasema kuwa mikopo yote inayoendelea kukopeshwa kwa mtu mmoja mmoja muda wa kurudisha mkopo ni wa miezi 6 mara kuanzia tarehe ya mkopo rudishwa,"amesema Choga.
Amesema baadhi ya maeneo yanayoendelea kufikiwa na mikopo hiyo ni Solo la Kariakoo ,Machinga Complex, Soko la Bog Brother, Solo la Feli, Maeneo ya Tabata Muslim .
Maeneo mwengine ni Tazara Vetenal ambapo imetajwa kuwa kila mmoja aliyepata mkopo huo kwa mwaka jana pia alikuwa tayari amekata Bima ya kujilinda na manjanga endapo itatokea ajali ya moto katika bidhaa zake nk.
Pia kiongozi huyo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kwani amekuwa akitoa maelekezo maalum ya kuweza kuyalea makundi ya machinga na bodaboda
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki hiyo Dkt Ibrahim Mwangalaba wakati kuelezea ufanisi na utendaji kazi wa Benki hiyo kwa mwaka 2022.
Dkt Mwangalaba amebainisha kuwa faida hiyo imetokana na ukuaji wa jumla wa mapato kwa asilimia 22 mwaka hadi mwaka kutoka shilingi za kitanzania Bilioni 12.8 hadi shilingi za kitanzaniaBilioni 15.6 mwaka 2022.
Aidha Mkurugenzi huyo wa Benki ya Maendeleo Plc aliendelea kusema kwamba mwaka 2022 benki hiyo imewakopesha Wafanyabiashara ndogondogo wapatao 2500,ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 3. zimetumika kwa ajili ya mikopo hiyo.
0 Comments