Header Ads Widget

VIONGOZI WA DINI YA KIISLAMU MALINYI WAUNGANA NA SERIKALI KUPINGA USHOGA, USAGAJI.

 



Sheikh mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sheikh Mohammed Ahmad Mwinyi ameungana na viongozi wengine wa serikali katika wilaya hiyo kulaani na kupinga vitendo vya ushoga na usagaji.


Sheikh Mwinyi ametoa kauli hiyo wakati wa Iftari kwa waumini na viongozi wa dini ya kiislamu Wilayani Malinyi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo April 19 ,2023.


Ameungana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mheshimiwa Pius Mwelase na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hamis Kitambuliho ambao walikemea vitendo hivyo na kutaka vyombo vya usalama kuanza kuwachukulia hatua wote wanaosadikika kufanya vitendo hivyo.



Sheikh wa Wilaya amesema waumini wa dini ya kiislamu na viongozi wote wanaungana kwa vitendo na Rais wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan kupinga vitendo vya ushoga na usagaji na kusema kuwa wataendelea kukema kwa nguvu zote Ili kuirudisha jamii katika maadili.


Awali Mwenyekiti wa Halmashauri ya Malinyi Mheshimiwa Mwelase aliwataka wazazi kusimamia maadili kwa watoto wao na jamii nzima kuwa waangalifi na kila misaada wanayopokea kujiridhisha kwanza kabla ya kupokea kama ina heri ama ina lengo baya kwa jamii.


"Ifikie wakati Sasa vyombo vya usalama kuanza kuwahoji Hawa wenye tuhuma za ushoga huko mitaani Ili kujiridhisha maana kuacha tu mtu anatuhumiwa kama anafanya vitendo hivyo bila kujua kweli ama sio kweli jamii yetu itaendelea kuharibika"alisema.



Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Malinyi Kitambuliho amesema wataendelea kupinga matukio hayo kwa kutoa Elimu kupitia idara ya maendeleo ya Jamii hasa kwa vijana ambao ndiyo waganga wakubwa wa matukio hayo.


Katibu wa Jumuiya ya wazazi ya Chama Cha Mapinduzi Thomas Liganga ambae alimwakilisha Katibu wa CCM wilaya ya Malinyi akitoa salamu za chama katika Iftari hiyo amesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa kukemea na kuwafundisha waumini kuhusu kukataa maasi hasa hili ya usagaji na ushoga.



Mbali ya viongozi wa dini ya kiislamu na waumini wa dini hiyo kuhudhuria Zifa hiyo pia watumishi wa Halmashauri pamoja na wadau wengine ni miongoni mwa walishiriki.


IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-H /W MALINYI.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI