UKARABATI wa sehemu ya barabara ya Chalinze Segera kwenye eneo la Kimange Wilaya ya Bagamoyo ambayo Aprili 15 ilimeguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha imemlazimu mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge kutembelea na kupongeza kukamilika ujenzi huo kwa wakati.
Akizungumza alipotembelea kujionea ukarabati uliokuwa ukifanyika kwenye eneo hilo ambalo limemeguka upande mmoja huku magari yakitumia upande mmoja kwenye barabara hiyo inayoelekea mikoa ya Kaskazini ambapo ilimlazimu Kunenge kutembelea kuona ukarabati uliokuwa unafanyika.
Kunenge alisema kuwa eneo hilo lilikuwa ni hatarishi kwani liko bondeni hivyo endapo zisingechukuliwa hatua za haraka ingeweza kuleta madhara makubwa kwa magari yanayotumia barabara hiyo kwani mvua bado zinaendelea kunyesha.
Kwa upande wake Meneja wa Tanroads mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage alisema kuwa kutokana na sehemu hiyo kumeguka imewabidi kuweka mawe na zege ili kuzuia mmomonyoko wa udongo ili usije ukaleta athari nyingine.
Naye Mkurugenzi wa Kampuni ya Link General Contractors Baltazar Malamsha alisema kuwa wanatum huuia utaalamu ili kuhakikisha eneo hilo halimeguki tena kwani mawe waliyoweka na zege vitaimarisha sehemu hiyo.
0 Comments