Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma
KUTOKANA na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa mawasiliano katika baadhi ya maeneo na kupelekea wananchi kukosa fursa mbalimbali za kijamii na kibiashara, serikali kupitia Shirika la mawasiliano Tanzania imeamua kuzitatua changamoto hizo kwa vitendo ambapo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Kampuni ya Huawei International imesaini Mkataba wa Upanuzi wa mkongo wa Taifa wa Mawasiliano .
Mkongo huo wa Taifa utafika katika Wilaya 23 nchini zenye jumla ya kilometa 1,520 wenye thamani zaidi ya bilioni 37 za kitanzania.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Nape Nnauye, amesema hayo leo jijini hapa kwenye hafla hiyo ya Utiaji saini mkataba wa upanuzi wa mkongo wa Taifa .
Waziri Nnauye amesema kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa kwa wananchi za kiuchumi, kwani Kasi ya upatikanaji wa mawasiliano yatachochea maendeleo Katika Wilaya hizo na Taifa kwa ujumla.
Amesema Serikali awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia suluhu Hassan Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu Bora ya mawasiliano yenye kutumia Teknolojia ya kisasa .
" Miundombinu hiyo ya Mawasiliano itakwenda kuleta tija na ufanisi katika kuongeza uzalishaji na ujenzi Wa uchumi pamoja na kuimarisha usalama na ulinzi Wa Taifa,"amesema waziri Nnauye
Amesema kuwa serikali imepanga kutekelwza Mradi Wa kuimarisha mawasiliano katika ngazi ya wilaya Kwa kuunganisha wilaya zote kwenye Mkongo Wa Taifa Wa amawailiano ili kuongeza Kasi ya upatikanaji Wa mawasiliano ambayo yatachochea Maendeleo katika wilaya na Taifa Kwa ujumla.
Aidha amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha Mkongo wa taifa wa Mawasiliano unasambaa nchi nzima na nchi zote zinapakana na nachinya Tanzania ambapo kwa sasa bado nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo mipango iliyopo ni kuifikia pia
"Kukamilika Kwa mradi huu Wa upanuzi Wa mkongo Wa Taifa Wa mawasiliano utasaidia kukuza matumizi ya TEHAMA na kuongeza Kasi ya upatikanaji Wa interneti yenye Kasi zaidi," Amesema Waziri Nnauye
Sambamba na hilo Waziri Nape ametoa rai katika maeneo yote yatakayopitiwa na mradi huo kuhakikisha wananchi wanapewa Elimu juu ya umuhimu wa miundombinu hiyo ili kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.
Mkurugenzi Mkuu Wa shirika hilo Mhandisi Peter Ulanga wakati akitoa TAARIFA ya shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL)amesema kuwa upanuzi Wa mkongo huo Wa Taifa Wa mawasiliano kwa wilaya hizo 23 ,unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita na utasaidia katika kukuza shughuli za kiuchumi, kibiashara, kijamii sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya wilaya na mkoa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Zuhura Muro amesema Serikali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwezesha utekelezaji wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenda kwenye ngazi ya Wilaya itachochea maendeleo ya kiuchumi na kusaidia serikali kukusanya mapato kwa njia ya mtandao.
0 Comments