Shirika la Tanzania Media for Maritime and Fisheries Development (TMFD) limeingia makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja na shirika la Mwanza Youth and Children Network(MYCN) katika nyanja mbalimbali ikiwemo, jinsia, haki za binadamu, afya na uezeshwaji wa jamii.
Makubaliano Hayo yaliyofanyika Leo April 5 katika ofisi za MYCN zilizopo Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mkurugenzi wa TMFD Bwana Edwin Soko amesema kuwa, hatua ni muhimu kwa kuwa TMFD inafanya kazi nyingi zinazoendana na shughuli zinazotekelezwa na MYCN hivyo ushirikiano huo utaongeza nguvu ya utendaji na utafutaji wa matokeo bora ya miradi.
Naye Mwenyekiti mtendaji wa shirika la MYCN Bwana Brightius Titus amesema kuwa, makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja yataleta ufanisi kwenye kutekeza malengo ya mipango iliyowekwa kwa mashirika yote mawili na kupunguza changamoto za watoto na vijana.
Moja ya makubaliano hayo ni kutafuta miradi kwa pamoja, kutekeleza miradi, kufanya tathimini ya miradi na kutoa taarifa ya miradi kwa pamoja.
0 Comments