NA HADIJA OMARY-LINDI........
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim ameiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kufanya ufuatiliaji wa nyaraka za mradi wa bweni la wanafunzi wenyemahitaji maalumu uliogharimu kiasi cha milioni 110 katika shule ya msingi Mtanga Wilayani baada ya kubaini uwepo wa kasoro hasa katika eneo ya stoo.
Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo Kaim alisema baada ya kufanya ukaguzi wa mradi huo ukaguzi wa nyaraka za mradi mwenge wa uhuru umebaini kuwepo na kasoro ndogondogo ambazo azikuangalia umakini kwenye eneo la stoo pamoja na mradi wenyewe.
Alisema hali hiyo imezifanya mbio za mwenge wa uhuru kutilia mashaka mradi huo na kumuagiza kamanda wa TAKUKURU wilayani kilwa kufanya uchunguzi wa kina katika nyaraka hizo na kwamba endapo watagundua tatizo basi mtumishi aliehusika awajibishwe kwa mujibu wa sheria.
“ hivyo mbio za mwenge wa uhuru pamoja na kazi kubwa ambayo imefanyika na ili kujilizisha zinamuagiza kamanda wa TAKUKURU kupitia mkuu wa wilaya akukabidhi zile taarifa ili kujirizisha kwa utaalamu wenu na endapo mtagundua kama kunatatizo muhusika anatakiwa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria” alisema Kaim
Akisoma taarifa ya ujenzi wa mradi huo mwalimu mkuu wa shule ya msingi mtanga Omari Naise alisema shule hiyo ni miongoni mwa shule zilizobahatika kupata mgao wa fedha za sherehe ya uhuru mwaka 2022 zilizobadilishwa matumizi na Rais Samia .
Aidha ameeleza kwamba lengo la mradi huo ni kutoa huduma ya malazi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo bweni hilo 1 linavyumba 20 na uwezo wa kuhudumia wanafunzi 80 kwa pamoja.
Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christophar Ngubiagai alisema pesa hizo zilitolewa na Rais Samia baada ya kuona changamoto zinazowakabili watoto hao wenye mahitaji maalumu ndipo alitoa kiasi hiko cha pesa kwa ajili ya kuwasaidia watoto hao.
Hata hivyo Ngubiagai alieleza kuwa baada ya kukamilika kwa mbweni hilo sasa watoto wenye mahitaji maalumu kutoka katika maeneo hayo ya kilwa pamoja na wale wa maeneo ya jirani watapata nafasi ya kwenda kusoma katika shule hiyo.
0 Comments