Header Ads Widget

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE APANDA MITI CHANZO CHA MAJI KIRANJERANJE KUHIFADHI MAZINGIRA

 



NA HADIJA OMARY LINDI..



KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim ametembelea chanzo cha maji kiranjeranje pamoja na kupanda miti ikiwa ni kuunga mkono jitihada za wananchi wa kijiji hiko za kuhifadhi mazingira katika chanzo hiko ili kiwe endelevu.



Akizungumza Mara baada  kutembelea , kuona mradi huo na kupanda miti Kaim amewapongeza wananchi wa kijiji hiko cha kiranjeranje kwa uhifadhi mzuri wa vyanzo vya Maji kwa kuwa  hata kauli mbiu ya mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 ujumbe wake unahamasisha uhifadhi wa mazingira na utunzaji wa vyanzo vya Maji ili kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia kauli mbiu isemayo "tunza mazingira okoa vyanzo vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na Uchumi wa Taifa"



Awali akitoa taarifa ya mradi huo wa upandaji miti kaimu meneja wa Ruwasa Wilaya ya Kilwa  Ramadhani Mabula alisema Eneo la chanzo hicho cha Maji linaukubwa wa mita za mraba 7,566 Sawa na ekari 1.87  linamilikiwa na kutunzwa na kijiji cha Kiranjeranje.




Alisema   kutokakana na mabadiliko ya tabia nchi ,shughuli za kibinadamu zinazofanywa na wananchi hao na kwa kuzingatia kuwa ni chanzo pekee cha Maji katika kijiji hicho wananchi hao wameamua kutunza na kujifadhi kwaajili ya kizazi kilichopo na kijacho ambapo jumla ya miti 556 imepandwa katika eneo hilo.



Hata hivyo mhandisi Mabula alieleza kuwa  eneo hilo lina Kisima kilichochimbwa mwaka 1954 Chenye uwezo wa kutoa Maji lita 1200 na kuweza kuwahudumia wakazi wapatao 11,000.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS