Header Ads Widget

MWENGE WAAGIZAJI MAREKEBISHO YA MILANGO NA MADIRISHA KITUO KIPYA CHA AFYA USUKA WANGING'OMBE

 


Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mwenge wa Uhuru umekagua,kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 9 ya maendeleo wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe pamoja na kutoa ujumbe wa mwenge wa uhuru.


Akipokea mwenge huo toka kwa mkuu wa Wilaya ya Makete Juma Sweda,mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta amesema Miradi hiyo inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.3.


Katika kituo Cha afya Makoga Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dkt.Mario Chota amesema zinatolewa huduma  mbalimbali pamoja na kutoa elimu ya Malaria,Lishe,Ukimwi na kupima virusi vya Ukimwi.



Aidha wataalamu wa afya wa kituo hicho wamesema kumekuwapo kwa mafanikio makubwa ya utoaji elimu hiyo kwani jamii inahamasika kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.


Kwa Upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru  kitaifa mwaka 2023 Ndugu Abdalah Shaibu Kaim amepiga marufuku tabia ya kukumbatia mila potofu zilizopo miongoni mwa jamii na kuwataka kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.



Hata hivyo amewaagiza wataalamu wa ujenzi kufanya marekebisho ya milango na madirisha katika kituo kipya Cha afya  Usuka kilichowekwa jiwe la msingi na Mwenge huo.


Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Wanging'ombe akiwemo Sela Mgeni wameshukuru kwa kujengewe kituo hicho Cha afya na kwamba huduma zinazotolewa zimekuwa msaada mkubwa kwao.



April 29 Mwenge wa Uhuru unakabidhiwa katika halmashauri ya wilaya ya Njombe

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI