Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma amewataka wakuu wa wilaya za Ruangwa, Nachingwea na Liwale Mkoani Lindi zinazounda ushirika wa chama kikuu cha ushirika (RUNALI) kusimamia kwa umakini na kuwekeza jitihada kubwa katika zao la korosho na ufuta katika Halmashauri zao ili yaweze kuongeza mapato ya Halmashauri hizo.MWANDISHI HADIJA OMARY MATUKIO DAIMAAPP,LINDI
Ngoma ameyasema hayo katika mkutano mkuu wa 6 wa chama kikuu cha RUNALI alipokuwa akifunga mkutano mkuu ambao umefanyika leo April 20 2023 huku akiwasisitiza wakurugenzi wa Halmashauri za Ruangwa,Nachingwea na Liwale kuwasimamia na kutetea masilahi ya wakulima ili kudumisha uhai wa halimashauri zao
‘’ Nje ya mapato ya ufuta na korosho hakuna Halmashauri ya Liwale ,Ruangwa wala Nachingwea mazao hayo ndio Maisha kwenye Halmashauri zetu hivyo ma DC tunapaswa kuwatizama na kuwasimamia wakulima vizuri kwani wakishindwa kuzalisha halimashauri zitayumba’’amesema Ngoma
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Liwale Goodluck Mlinga amewataka viongozi wa vyama vya msingi kuwa waaminifu katika malipo ya wakulima kwakua atatumia vyombo vya dola pale itakapobainika viongozi hao “kupiga” fedha za wakulima.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo amewataka viongozi wa Amcos kuunda SACOS zitakazosaidia kuweka akiba na kukopa ili kuweza kusaidia kuwavutia wakulima wengi kujiunga katika vyama vya msingi kukwepa biashara ya kangomba inayowaumza wakulima wengi.
Hata hivyo aliwataka viongozi hao kujali masilahi ya mkulima ili kilimo cha mazao ya korosho,ufuta,alizeti na mbaazi kiwainue wakulima kwa kuwa Ushirika ni biashara.
Kaimu mkurugenzi Halmashauri wilaya ya ruangwa DHRO Maisha Mtipa amesema ushirikiano wa vyama vya msingi Amcos na chama kikuu cha ushirika RUNALI ni jambo la msingi linalo imarisha na kustawisha halimashauri hizo hivyo amehimiza ushirikiano ili kuwahudumia wananchi kwa tija huku.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya chama kikuu cha ushirika Runali , mwenyekiti wa chama hiko Odas Mpunga alisema kuwa ili kuendelea kuwa imara Chama hiko kinadhamilia kujiimarisha kwenyekuongeza uzalishaji wa mazao mbali mbali mbali ya Biashara.
"Kuanzisha shamba kwa ajili ya kuzalisha mbegu na kuziuza kwa wakulima wetu kwa bei nafuu, tunataka pia kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kila mwana ushirika hadi watumishi wa RUNALI kuwa na hekari zisizopungua mbili za ufuta, mikorosho na alizeti pamoja na kuwepo kwa utaratibu kugawa pia mbegu za alizeti pia kwa vyama wanachama ambapo katika hili pia tutaingia mkataba wa uzalishaji kwa kusaidiana na maafisa ugani wetu" alifafanua Mpunga
















0 Comments