Header Ads Widget

DC KALI ABAINI TAASISI YA YES WE CAN KUJIHUSISHA NA USHOGA

 


Mkuu wa wilaya Kigoma Salum Kali (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Yes We Can Emerson  Mpenda (kulia) wakati wa ukaguzi kwenye vituo vya taasisi hiyo vinavyotuhumiwa kutoa mafunzo ya ndoa za jinsia moja na ushoga


Na Fadhili Abdallah,Matukio DaimaAPP,Kigoma

MKUU wa wilaya Kigoma Salum Kali akiongoza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo amefanya ukaguzi wa ghafla kwenye vituo vya Taasisi isiyo ya kiserikali ya Yes We Can na kubaini kuwepo kwa dalili ya taasisi hiyo kuendesha shughuli zinasadikiwa kuwa na mahusiano ya ndoa za jinsia moja na ushoga

Katika ukaguzi huo Mkuu huyo wa wilaya aligundua kuwepo kwa picha, michoro, vitabu na mafundisho mbalimbali yanayoashiria kuwepo au kufundishwa kwa  vitendo hivyo.

Kufuatia hali hiyo Mkuu huyo wa wilaya amemkamata Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Emerson  Mpenda kwa ajili ya mahojiano zaidi na kutoa taarifa za tuhuma hizo sambamba na tuhuma za kuhifadhi wanafunzi kutoka nje ya wilaya kwa madai ya kutoa elimu ya ziada (Tuition).


Vitabu vilivyokutwa kwenye kituo cha Yes We Can ambavyo vinadaiwa kupigwa marufuku


Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa uvamizi na ukaguzi huo umekuja baada ya kupokea taarifa za tuhuma za kuwepo kwa taasisi hiyo ikiendesha shughuli zake tofauti na usajili wa uundwaji wa taasisi hiyo.

Aidha katika ukaguzi huo Mkuu huyo wa wilaya amebaini shirika hilo kuwa na wageni kutoka nchi za Ulaya ambao taarifa zao hazijulikana vizuri wakifundisha mambo mbalimbali kwenye kituo hicho lakini taarifa zinaonesha kwamba wamekuja kwa shughuli za utalii.

Awali Mkurugenzi wa Taasisi ya Yes We Can, Emerson Mpenda alisema kuwa taasisi  yake imesajiliwa kama shirika lisilo la kiserikali linalotoa elimu na huduma za ufundi kwa wanafunzi masikini.

Alisema kuwa wamekuwa wakitembelewa na marafiki zao kutoka nje ya nchi na hawatoi elimu ya masuala ya ushoga 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI