Header Ads Widget

CHAMA CHA ADC KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI CHATAKA BUNGE KUTUNGA SHERIA KALI KUWABANA MASHOGA


 CHAMA  cha  Alliance for Democratic Change (ADC) kanda  ya  nyanda  za  juu  kusini  kimeshauri  wabunge  kutunga  sheria kali  itakayokomesha   vitendo  vya  ushoga na ndoa za  jinsia  moja hapa  Nchini.


Huku  kikiwataka  mawaziri  waliotajwa  kuhusika na  ubadhilifu  wa  fedha  za  umma  kujiuzulu nafasi  zao   ili  kupisha  uchunguzi ufanyike kama  sehemu ya  kumsaidia Rais Dkt  Samia  Suluhu Hassan katika kuliongoza Taifa bila  ya  ufisadil.

Akizungumza  leo  katika  kipindi  cha Press  leo  kinachorushwa na chanel  ya  matukio Daima  Tv  kamishna  wa ADC kanda ya  nyanda  za juu kusini Daus Masasi alisema  kuwa  pamoja na mambo mazuri  yanayofanywa na  serikali  iliyopo madarakani  chini ya  Rais  Dkt  Samia Suluhu Hassan  ila  yapo  mambo  ya  makwazo na kilio  kikubwa kwa  Taifa  kama  janga  la Ushoga ,Usagaji na  ndoa  za  jinsi moja ambalo   mwarubaini  wake ni wabunge kutunga sheria kali  itakayokomesha  vitendo hivyo .

“ Hawa  wabunge  wasilalamike kama  tunavyolalamika   sisi  wananchi  maana  wao  ndio  wenye nafasi kubwa ya  kukomesha tatizo  hili kwa  kulitungia sheria  kali  ambazo  zitaliepusha  Taifa na janga  hili sasa  kama  wabunge  hao  wanalalamika  nani atalifanyia kazi  hili “

Alisema  kuwa   lazima  wabunge  kusimama  kwa  pamoja  kupinga suala  hili la  ndoa  za jinsia  moja  kwa  kulitungia  sheria  kali kama  ambavyo  bunge la Uganda  na  serikali yake ilivyopitisha   sheria  kali ya  ushoga na ndoa  za  jinsia  moja .

Masasi  alisema   ripoti ya Dkt  Harrison Mwakyembe  imetaja  wazi  wazi mashirika  ambayo  yamekuwa  yakihamasisha  vitendo vya ushoga  lakini mashirika  hayo  wizara ya  afya  inayatambua na ndio  ambayo  inayasimamia  sasa  ni  vizuri wizara   kuchukua hatua  za haraka  ili  kulinusuru  Taifa na janga   hilo  kubwa .

 

Pamoja na  kutaka  wabunge  na  wizara  ya  afya  kuchukua  hatua  kulinda Taifa  bado alishauri  kumbi  za  starehe kuanza  kufuatiliwa kwa karibu  ili  kuwakamata na  kuwachukulia  hatua  za  kisheria   wale  wote  wanaojihusisha na uhamasishaji  wa  vitendo visivyo na maadili  kwa  Taifa .

Katika  hatua  nyingine  Masasi  alipongeza  ripoti ya  CAG  kwa  kuonesha  mapungufu  katika  usimamizi  wa   fedha  za  miradi ya maendeleo  na  kuwa  wote  waliohusika na mapungufu hayo  wanapaswa  kumsaidia  Rais Dkt  Samia  kwa  kukaa pembeni  ili  kuruhusu  uchunguzi  ufanyike  na  ikibainika  wamehusika katika  ulaji  wa  fedha  za  umma basi sheria  zichukuliwe  dhidi yao  pasipo  kujali  nafasi  za uongozi  walizokuwa  wakizitumikia .

 

Pia   wabunge  kuacha unafiki katika  suala la ripoti ya  CAG  maana  wengi  wao  wanachuki  binafsi na  baadhi yao  walipata  kuwa mawaziri  ila  leo ndio  wakosoaji  wakubwa  wa serikali .

 

Kuwa suala la  wizi  wa  fedha za umma  halijaanza  leo  bali  lilikuwepo  miaka  yote  isipo  kuwa kipindi  hiki  cha Rais Dkt  Samia  kumekuwepo  uwazi  mkubwa  wa utoaji  wa taarifa ya CAG.

Alisema  kuwa  kupitia   fedha  zilizopotea kwa  wachache  kuzembea katika  usimamizi  kulikuwa na  uwezekano  wa  Watanzania  kupata   huduma  za  afya   kwa  gharama  ya  fedha   hizo  za umma.

 

Aidha   Masasi  alimshauri Rais Dkt  Samia  katika teuzi zake mbali mbali  za  wabunge na  wakuu  wa wilaya na mikoa kutoa nafasi  kwa  watu  kutoka  vyema  vya upinzani  ili  kuongeza nguvu ya  usimamizi  wa  fedha  za umma na  kuisaidia  serikali katika utendaji kazi  wake .

Alisema kuwa  tofauti ya Rais  Dkt  Samia na wengine  waliotangulia ni moja  kubwa ambapo  Dkt  Samia  amekuwa akitanguliza  huruma  ya mama katika kuwahudumia  watanzania  huku  mchwa  wachache  wameendelea  kumkwamischa  ndoto  zake  za  kulitumikia Taifa .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI