Mtaji wa wanahisa wa Benki ya Ushirika Kilimanjaro ( KCBL) umeongezeka na kufikia Shilingi bilioni 4.4 kutoka shilingi Bilioni 2.7 kwa kipindi cha miaka miwili hali ambayo imetajwa kama mafanikio makubwa katika kuimarisha benki hiyo.
Akizungumza katika mkutano na vyombo mbalimbali vya habari Meneja mkuu wa Benki hiyo ya KCBL Godfrey Ng’urah amesema benki hiyo ambayo ilikuwa imeyumba kwa miaka mitatu kwa sasa imesimama na inapiga hatua kubwa na kusema ifikapo mwishoni mwa mwezi June Benki hiyo ya KCBL inatajiwa kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika.
Ng’urah amesema moja ya mafanikio hayo kwa mwaka 2022 ni kuongezeka kwa akaunti mpya zinazofanya miamala za wateja kufikia Elfu 21 kutoka Akaunti 15 za mwaka 2021, mtaji wa wanahisa umefikia Shilingi bilioni 4.4 kutoka Shilingi bilioni 2.7 za mwaka 2021, mikopo ya wateja imekuwa kwa asilimia 59, na kufikia Bikioni 7.5 ukilinganisha na Bilioni 4.7 ya mwaka 2021 ,huku akisema mapato ghafi ya benki yameongezeka kwa asilimia 25 kufikia bilioni 1.5 kutoka milioni 1.2 kwa mwaka 2021 kama anavyo eleza.
Benson Ndiege ni Mrajisi wa vyama vya Ushika Nchini amesema bila kuficha, hapo awali walikuwa na watendaji ambao hawakuwa na weledi licha ya changamoto ya kibiashara walifanya Ubadhirifu pamoja na wizi katika benki hiyo, huku akiupongeza uongozi uliopo kwa kufanya kazi kwa uwazi na uadilifu na kusema kwa sasa hakuna mtu yoyote atakaye weza kugushi kwani taarifa zote zipo .
Hata hivyo Meneja wa Benki hiyo ya KCBL Godfrey Ng’urah amesema katika mchakato huo wa kuwa Benki ya Taifa ya Ushirika , Benki ya KCBL inashirikiana na Tume ya Maendelelo (TCDC) Benki ya CRDB, SCCULT,TFC, na vyama vya ushirika ili kufanya mageuzi ya kimfumo na uendeshaji ndani ya Benki hiyo.
0 Comments