Zaidi ya watu sita wameuwawa kwa kushambuliwa na Mamba katika kata mbalimbali za Halmashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza ikiwemo kata ya Nyakasasa.
Hayo yamebainishwa na madiwani katika mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha robo ya pili ( Oktoba – Disemba ) , 2022/2023
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Mwita Mirumbe amesema, halmashauri itachukua hatua ikiwemo kutoa vibali kwa ajili ya kuwasaka na kuwauwa mamba hao.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga ameliomba baraza la madiwani la halmashauri ya Buchosa kuhakikisha linasimamia ukusanyaji wa mapato ya halmashauri ya Buchosa.
0 Comments