Msafiri Nzunuri Afisa Maendeleo ya jamii sekretariet ya mkoa Kigoma akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa mradi wa afya yangu unaotekelezwa na Shirika la KIVIDEA
Na Fadhili Abdallah,Matukio DaimaAPP Kigoma
Wazazi na jamii wametakiwa kuwaandaa watoto wao na vijana ili kuwa nguvu kazi na hazina kubwa ya taifa kwa siku za baadaye kwani jambo hilo likishindwa kufanyika sasa watoto na vijana hao watapotea na mchango wa vijana kwa Taifa hautakuwepo.
Afisa Maendeleo ya jamii katika sekretariet ya mkoa Kigoma,Msafiri Nzunuri alisema hayo akizindua awamu ya pili ya mradi wa afya yangu nguvu yangu unaotekelezwa na Shirika la maendeleo ya vijana Kigoma (KIVIDEA) kwa ufadhili wa Shirika la Terre des Hommes Schweiz (tdhs) la nchini Uswiss.
Nzunuri alisema kuwa vijana wanazo changamoto nyingi na mahitaji mengi kulingana na akili zao, ukuaji na makundi rika hivyo ni vizuri malezi na makuzi ya vijana yakasimamiwa kwa karibu ikiwemo kuwapa taarifa ambazo zitaatarisha afya zao, kuwapa ujuzi na stadi ambazo zitawafanya kuwa mtaji kwa familia na taifa.
Afisa maendeleo ya jamii huyo ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma alisema kuwa serikali na taasisi zisizo za kiserikali zina mipango mingi katika kuwasimamia vijana hivyo ni vizuri wazazi, serikali na wadau mbalimbali wakashirikiana pamoja ili kuhakikisha malezi ya vijana hao yanasimamiwa vizuri.
Awali akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi huo Meneja Miradi wa Shirika la KIVIDEA, Jaquiline Kitema alisema kuwa mradi huo utatekelezwa katika kata 19 za Halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji na kata nne za halmashauri ya wilaya Uvinza ambapo vijana 12,840 ndani na nje ya shule watafikiwa.
Meneja Mradi huyo alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo vijana 4148 watafikiwa moja kwa moja ambapo vijana wengine 12,840 watafikiwa na vijana wenzao ambapo kwa jumla ya watu 24,756 watafikiwa na mradi huo wakiwemo wazazi,walimu na maafisa wa serikali wanaosimamia elimu na maendeleo ya
vijana.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la KIVIDEA, Babu Pascal alisema kuwa vijana wana changamoto kubwa katika malezi na makuzi yao hivyo jamii inapaswa kusimama nao na kuwapa mwelekeo wa namna ambavyo wanapaswa kuishi ili kuvuka umri wenye changamoto kubwa.
Mkurugenzi huyo alisema kuwa vijana na watoto wakipewa elimu ya afya ya uza zi, stadi za maisha, masuala ya ukatili.
0 Comments