Header Ads Widget

WAUGUZI NA WAKUNGA WATAKIWA KUZINGATIA MAADILI WAWAPO KAZINI ILI KUWAPA WANANCHI HUDUMA BORA

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Dkt,Seif Shekalaghe amewataka wauguzi na wakunga kuhakikisha kuwa wanazingatia maadili na taaluma (Professionalism) ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.


Akizungumza jiijni Dodoma leo katika ufunguzi wa kikao cha wauguzi na wakunga Dkt,Shekalaghe alisema kuwa wauguzi ni watu muhimu sana katika sekta ya utoaji huduma za Afya kwa jamii kwa kuwa wao wapo katika hatua ya mgonjwa kuingia hospital mpaka anapotoka.


“Mgonjwa akifika hospitali ili akamuone Dkt lazima apelekwe na muuguzi, na anapotakiwa kulazwa ni muuguzi anayemuhudumia, na kumfutilia Shinikizo la Damu (pressure ) huku huduma nyingine zote zinafanywa na wauguzi” amesema.


Dkt Shekalaghe pia amewataka wahudumu na wakunga kuhakikisha kuwa huduma kwa wateja zinatolewa kwa ubora kwa kuzingatia maelekezo yote yaliyo katika maadili pamoja na viapo vyao vya kazi.


“Ninaongea na wauguzi na wakunga 280 ambao ni wawakilishi wa wauguzi na wakunga 42,000 waliosajiliwa na chama cha wauguzi na wakunga Tanzania, niwatake nendeni mkasimamie maadili ya kazi yenu, nyie ni jeshi kubwa sana katika sekta ya huduma ya afya, nyie ndio mnaobeba taswira ya Taifa katika sekta ya afya” anesema.


“Watu wanataka tuwafundishe customer caring, lakini uwajali wagonjwa, haya mambo ya customer caring yako katika code of ethics zenu na mnaapa kila mwezi hivi viapo vya kila mwezi ni kuwakumbusha nini mnatakiwa kufanya maana mambo yote kuhusu huduma kwa wateja yako humo” aliongeza.


Dkt shekalaghe pia amewataka wahudumu na wakunga kuendelea kuwa wamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma kwa ubora.


“Niwaombe mpendane, mshirikiane na kufanya kazi as a team work, hii itawasaidia kutatua baadhi ya changamoto lakini pia mtaweza kufanya vizuri zaidi, upendo hujenga umoja”amesema.


Na kuongeza Kusema “Ninaposema mpendane na kushirikiana ni pamoja na katika semina kama hizi, ukija ukitoka nenda waited watu wa department yako wambie ulichojifunza, lakini pia kuwe na utaratibu wa kubadilishana sio kila kikao ama semina," amesema 


Kikao hicho cha siku tano kimewakutanisha wauguzi na wakunga 280 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania Bara waliosajiliwa na baraza la wauguzi na wakunga.



Naye Mkurugenzi wa huduma uchunguuzi na ukunga wizara ya afya Ziada Sellah,amesema kuwa kikao hicho ni kwa ajili ya kujifunza mamboa mbalimbali ikiwemo maadili na kutatua changamoto.


Aidha amesema,malengo hayo pia ni pamoja na kujadili huduma ya uuguzi na ukunga na changamoto za watumishi zinazohusu utoaji wa huduma zinazojali mtu heshima na kwa upendo.


"Baada ya kikao hiki ambacho kitakuwa cha siku tano tutakapotoka hapa  watakuwa wamepata majibu ya changamoto ambazo zitakazoleta  mabadiliko chanya kwa faida ya serikali na wananchi wake"amesema


Naye Mwenyekiti wa waauguzi wakuu wa mikoa ya Tanzania bara,Alhaj Ahmed Chibwana amesema bado kwenye upande wa waauguzi wanakabiliwa na changamoto ikiwemo za kutofanya kazi zao kwa mujibu wa kiapo chao 



Amesema kuwa wapo baadhi ya waauguzi wamekosa maadili na ueldi,lakini hili ni kutokana na kuongezeka kwa wingi wa kazi na kukosa vitenda kazi ya idadi ndogo waliyo kuwanavyo.


"Wingi wa kazi na ukosefu wa vitendea kazi pia inawalazimu wakati mwingine kuonekana wauuguzi hao hawafanyi kazi zao kwa maadili,hali ambayo imekuwa ikimlazimu hata mgonjwa wakati mwingine kuchangia mwenyewe madawa"amesema.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI