Header Ads Widget

WATOA HUDUMA KWENYE MIGODI YA MADINI WAENDELEA KUBORESHEWA MAZINGIRA YA KAZI

 



 Greyson Mwase na Mwanahamisi Msangi, Arusha


Kamishna wa Madini kutoka Wizara ya Madini, Dkt. Abdulrahman Mwanga amesema kuwa Serikali kupitia Wizara ya Madini itaendelea kutatua changamoto kwa watoa huduma kwenye shughuli za utafiti na uchimbaji wa madini ili kuhakikisha watanzania wote wananufaika na uwekezaji katika Sekta ya Madini ili sekta hiyo iendelee kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.


Dkt. Mwanga ameyasema hayo leo Machi 15, 2023 kwenye Jukwaa la Pili la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini linaloendelea jijini Arusha linalokutanisha kampuni za uchimbaji wa madini, watoa huduma wa madini kwenye migodi ya madini na Taasisi za Kifedha.


Amesema kuwa ili kuhakikisha watanzania wote wananufaika na rasilimali za madini nchini, Serikali imeendelea kuboresha Sheria za Madini ikiwa ni pamoja na Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 yenye lengo la kuhakikisha kila mtanzania kwa namna moja ama nyingine anashiriki kwenye uchumi wa madini.


Amesema kuwa, kama mkakati wa kutatua changamoto za watoa huduma kwenye migodi ya madini, Serikali kupitia Tume ya Madini imekuwa ikitoa elimu kwa wadau wa madini ikiwa ni pamoja na majukwaa mbalimbali yenye lengo la kubadilishana uzoefu, kujadiliana changamoto mbalimbali pamoja na kuzitatua.



Katika hatua nyingine, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele kwa uhamasishaji wa Serikali kuendelea kufanya kazi na Sekta Binafsi na kuongeza kuwa Wizara ya Madini chini ya Waziri wake, Dkt. Doto Biteko imeendelea kukutana na wawekezaji binafsi, taasisi za kifedha na kuwaunganisha na kampuni za madini ili kukuza uwekezaji katika Sekta ya Madini.



Aidha, ameipongeza Tume ya Madini kwa mwendelezo wa majukwaa na mikutano mbalimbali ambayo imekuwa ikifanyika mara kwa mara kama lengo la kuelimisha wadau wa madini kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini.


Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini kutoka Tume ya Madini, Venance Kasiki akielezea lengo la jukwaa hilo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI