Header Ads Widget

SIMBA SC WATIA KAMBI TANDIKA KWA HAMASA KUELEKEA MCHEZO WA KIMATAIFA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA DHIDI YA HOROYA

 



Na:Dickson Bisare Matukio Daima TV Dar es salaam.



UONGOZI wa Simba Sc umezindua wiki ya hamasa Tandika kuelekea mchezo wa  Kimataifa kati ya timu ya Horoya Sc utakaopigwa siku ya Jumamosi ya tarehe 18/3/2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium jijini Dar es salaam.



Akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi huo wa hamasa kuelekea mchezo huo Afisa Habari wa timu hiyo Ahmed Ally amesema



"Wanatandika leo tupo hapa Gongo la Mboto kwa jambo moja tu ambalo ni kuja kuwambia kwamba siku ya jumamosi ya tarehe 18/3/2023 tutakuwa na jambo letu moja tu pale kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium jijini Dar es salaam,nalo ni kutinga hatua ya robo fainali kwa mara nne mfululizo,hivyo niwaomba wanasimba wote wa hapa Tandika Gongo la mboto mjitokeze kwa wingi siku hiyo kwani tunaenda kufanya makubwa."




Sambamba na hilo msemaji huo ameendelea mbele na kusema timu ya Horoya Sc wamejichanganya wanatakiwa tu wajue kwamba hatutakubali hata chembe wao kuondoka na hata alama moja.Pointi zote tatu wataziacha hapa nyumbani na ni pale uwanja wa Benjamin Mkapa Stadium.



Naye,Katibu wa tawi la Simba Sc (Pugu Mnadani) Mswazi Timotheo amewashukuru Simba Sc kwa uongozi mzima kuweza kuwafikia katika tawi lao.Mwenyekiti ndugu Mswazi Timoteo ameendelea mbele na kusema wao kama mashabiki wa timu ya Simba sc wapo tayari kufa kuwa mashabiki wa timu ya Simba sc siku ya jumamosi kwa mkapa timu ya Horoya wanaenda kunyolewa na kuweza kuacha alama tatu ambazo zitakuwa ni muhimu kwetu sisi kuweza kufika hatua ya robo fainali. 




Naye, msemaji wa timu ya Simba Sc ameendelea mbele baada ya kufika katika eneo la Pugu Mnadani na kuweza  kuongea na mashabiki wa timu ya Simba katika eneo hilo na kuweza kusema.


"Siku ya Jumamosi ni siku kubwa kwetu na tunaamini lazima alama tatu zibaki nyumbani siku hiyo,robo fainali tunaitaka kwa mara nne mfululizo kwani ndiyo haja yetu kubwa kama timu ya Simba Sc." 




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI