Header Ads Widget

WAKULIMA WASHAURIWA KUTUMIA WATAALAMU TARI

 



Mratibu wa Program ya zao la Ufuta Kitaifa Joseph Nzunda amewataka wakulima kuutunza ufuta vizuri kwakufuta ushauri wa watalaamu ili kuondokana vijidudu visumbufu katika zao hilo.


Akizungumza na wakulima katika Wilaya ya Mtwara alisema kuwa maeneo mengi ya kata hiyo na kata ufuta umeathiriwa na visumbufu ambavyo vinapaswa kuondolewa kwa kupuliza dawa za viadudu hivyo kwa ushauri wa watalaam.


“Unajua ufuta ukianza kutoa maua hatushauri mkulima kutumia madawa kwanza yanaweza kuathiri mmea wenyewe na maua pia ambayo inaweza kuua wadudu wenye faida wanaosaidia kuchavusha maua”


“Usipotumia dawa mapema wadudu hao hubadilika  na kukua  ambapo huwa ni ngumu kuwadhibiti na pia dawa zake ni ghali kwenye manunuzi ni vema kumdhibti huyu anayekula majani katika hatua za awali”



“wakulima tunawashauri watumie mbegu bora ikwemo Lindi 202, Ziada 94 na Mtondo 2013 pia epukeni kutumia mbegu ambazo mmea ni mkubwa lakii mazao kidogo tumieni teknolojia na ushauri sahihi kutoka kwa wakulima ili kupanda mapema kuvuna kwa wakati ili kuepuka kupoteza ufuta shambani”


mashambaulizi ya mdudu huyu hushambulizi ya mdudu  huyu na husababisha  mmea wa ufuta kudhoofika  na kudumaa na wakati mwingine kunyauka na kufa kabisa” alisema Nzunda


Issa Juma Mwalinga Mkulima wa Ufuta Kata ya Kitere alisema kuwa amekuwa akitumia watalaamu ili kuweza kuboresha kilimo cha ufuta.


“Wakulima watumie watalaamu kupata ushauri ili tulime kisasa na tuondokane na mbegu za asili ambazo zinakuwa kubwa ndefu alafu mavuno kidogo nilipata elimu TARI mwaka 2018 lakini tunae afisa kilimo wa kata ya kitere anatusaidia sana ambaye anatupa ushauri mzuri”


“katika mbegu zote mtondo naiona iko vizuri yaani ikiwa chini futi nne tu unaanza kuona maua nasubiri mavuno ili nione ipi itanifaa na bora zaidi pia inastahiili magonjwa wadudu na ukame pia” alisema Issa



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI