Header Ads Widget

"US MONASTIR NI TIMU BORA WAMEKUJA TANZANIA KUCHEZA HAWAJAJA KUTALII" KOCHA WA YANGA




Na:Dickson Bisare Matukio Daima TV Dar es salaam.


Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Sc amesema kuelekea mchezo wa kesho wa Kimataifa shirikisho barani Afrika dhidi ya US Monastir leo jijini Dar es salaam utakuwa mgumu lakini maandalizi yako vizuri.



Akizungumza katika ukumbi wa TFF mbele ya wanahabari amesema kuwa mchezo wa kesho anatambua mchezo utakuwa mgumu dhidi ya timu ya US Monastir kwani anafahamu US monastir wanakikosa kizuri.



"Ninafahamu mchezo wa kesho utakuwa mgumu na timu ya US Monastir ni timu bora na wamekuja Tanzania kucheza hawajaja kutalii,hivyo basi nimeweza kuwaandaa wachezaji wangu vizuri kuelekea mchezo huo huku tukifahamu mchezo wa kesho ni muhimu kwetu sisi kuweza kuvuka h"atua inayofuata." Alisema Nasridinne Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc.



Sambamba na hilo, Nasdine Nabii ameendelea mbele na kusema anawaomba sana mashabiki wa timu ya yanga kesho waweze kujitokeza kufika uwanjani kwa wingi kwani shabiki ni mtu wa muhimu sana kwenye swala la mpira wa miguu.



"Ninawaomba sana mashabiki wetu wa yanga mnaipenda timu yenu niwaombe siku ya kesho muweze kujitokeza kwa wingi kujitokeza uwanjani,uwepo wenu uwanjani ni faraja kwetu na tunafahamu umuhimu wenu sana,lakini pia nipende kuipongeza timu ya US Monastir kwa kutumiza miaka 100 tangu kuasisiwa kwake,nafahamu jana imekuwa siku yao ya kusherehekea siku hiyo hivyo,nafahamu watacheza mpira kwa kujituma zaidi lakini sisi tunafanya tuwezalo ili tuweze kupata matokeo." Alisema Nasdine Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc. 



Wakati hayo yakijiri kocha wa Yanga ameendelea mbele kwa kujibu baadhi ya  maswali kutoka kwa wanahabari waliokuwa kwenye Ukumbi wa mikutano makao makuu ya TFF,Ilala jijini Dar es salaam swali likiwa kwa michezo ambayo imepita timu ya yanga imefungwa kwa magoli ya set peaces na hao US Monastir amesema.




"Tunawafahamu timu ya US Monastir wapo vizuri na tumewafuatilia kwa kuangalia baadhi ya "video" fupi wakiwa wanacheza na tumeona udhaifu wao upi wapi na kwa siku ya kesho naamini kwa nilivyowaandaa wachezaji wangu kuelekea mchezo wa kesho tutaenda kucheza na kuweza kushinda na kupata pointi tatu ambazo zitakuwa ni muhimu kwetu kama timu lakini pia kwa taifa kwa ujumla." Alisema Nasdine Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc 




Kuhusu taarifa ya mchezaji wa kigeni kutoka Ivory Coast ambaye amekuwa nje ya uwanja takribani kwa muda mrefu kwa kupatwa na majeraha Benard Morrison kocha ameelezea.



"Bernard Morrison ni kweli amekuwa nje kwa muda mrefu takribani miezi miwili nje ya uwanja,lakini amerejea uwanjani tutaendelea kumuangalia lakini pia Mshambuliaji Fiston Mayele lakini Kenendy Musonda tuliowapa mapumziko kidogo ila watakuwepo kwenye mchezo wa kesho," Alisema Nasdine Nabii Kocha Mkuu wa Yanga Sc.




Naye,Mwaakilishi wa wachezaji wa timu ya Yanga Denis Nkane ameongeza mbele ya wanahabari na kusema utayari wao kuelekea mchezo wa kesho kwani wanafahamu utayari wao na umuhimu wa mchezo wa kesho ili kuweza kuvuka kuelekea hatua ya robo fainali.



"Sisi kama wachezaji kwa ujumla tumejipanga na tupo tayari kuelekea hatua inayofuata,kwani tutakuwa tunaiwakilisha taifa lakini pia kwetu sisi kama timu kwa ujumla hivyo sisi tunahitaji pointi zote tatu ili tuweze kuvuka kwenye hatua ya robo fainali." Alisema Denis Nkane mchezaji wa Yanga Sc.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI