Header Ads Widget

TUTAENDELEA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUHUSU SHERIA- JAJI MFAWIDHI PAUL NGWEMBE

 


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro Mheshimiwa Jaji Paul Joel Ngwembe amesema mahakama kuu kanda ya Morogoro itaendelea kutoa elimu ya sheria kwa wananchi ili kupunguza makosa ya jinai ambayo yamekuwa na marudio kwa wananchi mara kwa mara.


Jaji Mfawidhi amesema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa kazi za mahakama wilaya ya Malinyi Machi 27 ,2023.


Ameyataja makosa ya kujirudia katika mkoa wa Morogoro kuwa ni ubakaji,matumizi ya dawa za kulevya,ulawiti na mashauri ya mirathi.



Amesema baada ya kufanya tathmini na kuona makosa hayo yana mtindo wa kujirudia wameamua kutoa elimu kwa wananchi wakitumia mbinu za mijadala ,makongamano na vyombo vya habari.


Alikuwa akitoa taarifa kwa kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya ya Malinyi inayongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Sebastian Waryuba wakati alipokutana na kamati hiyo katika ofisi za mkuu huyo wa wilaya pamoja na watumishi wa Mahakama hiyo.


Mahakama kuu kanda ya Morogoro imeridhia ujenzi wa mahakama ya kisasa katika Wilaya ya Malinyi ujenzi ambao unatarajia kuanza hivi karibuni.




Aidha amepongeza  utendaji kazi wa mahakama ya wilaya ya Malinyi kwa kuendesha keso kwa mfumo wa kielectoniki ambao umesaidia kupunguza mashauri katika mahakama hiyo ambayo inategemea mahabusu ya gereza la wilaya ya ulanga kuwatunza washtakiwa wanaonyimwa dhamana ama kukosa dhamana(umbali wa gereza hilo ni kilomita 180 kutoka Malinyi).


Akitoa taarifa ya utendaji wa mahakama ya Wilaya ya Malinyi Hakimu Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Samuel Jossia Obasi utendaji kazi wa mahakama ya wilaya ya Malinyi unakwamishwa na umbaliwa mahabusu ambao hulazimika kuja siku za kesi ama siku zingine kukosekana kutokana na changamoto mbalimbali .


Ameongeza sababu hizo za kuwakosa mahabusu mahakamani imewalazimu mashauri mengi kuendeshwa kwa mfumo wa kielektronik ambapo wamefanikiwa kumaliza mashauri kadhaa katika mahakama hiyo.



Katika ziara hiyo Jaji mfawidhi pia amepata nafasi ya kutembelea kiwanja cha mahakama ya wilaya ya Malinyi ambacho kinatarajiwa kujenga mahakama ya Wilaya ya Malinyi.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-H/W MALIN



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI