Header Ads Widget

" HAKUNA UINGIZWAJI WA MADAWA YASIOFAA NA MAGENDO KUPITIA KIGOMA" TMDA

 




Na Fadhili Abdallah,Kigoma


MAMLAKA ya dawa na vifaa tiba nchini (TMDA) imesema kuwa imejiridhisha kuwa hakuna uingizaji wa madawa yasiyofaa na magendo yanayoingizwa nchini kutoka nchi jirani kupitia mkoa Kigoma.


Mwenyekiti wa bodi ya TMDA, Eric Shitindi alisema hayo wakati wa ziara ya wajumbe wa bodi hiyo na uongozi kutembelea maeneo mbalimbali ya mkoa Kigoma kuona utoaji huduma wa maeneo yanayosimamia na mamlaka hiyo.


Katika ziara hiyo wajumbe hao wakiambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo na watendaji waandamizi wa mamlaka hiyo wamejiridhisha kwamba mkoa Kigoma ni salama dhidi ya uingizaji wa dawa bandia na zisizofaa.



Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TMDA, Adam Fimbo alisema kuwa mkoa Kigoma ni shwari dhidi ya uingizaji wa dawa bandia na za magendi na hiyo inawapa picha kwamba ushirikiano wa mamlaka mbalimbali za kiserikali unatekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kuzuia uingizaji wa dawa na vifaa tiba ambavyo haviruhusiwi.


Fimbo alisema kuwa mamlaka yake kwa sasa haina watendaji wanaosimamia suala hilo mkoani Kigoma  lakini linafanywa na mamlaka nyingine za serikali na kwamba wako mbioni kuhakikisha watendaji wa TMDA wanakuwepo ili kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali kusimamia suala hilo.


Akiwa hospitali ya mkoa Kigoma Maweni Mkurugenzi huyo ameeleza kuridhishwa na uanzishaji wa mpango wa uzalishaji wa gesi ya oksijeni kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kupumua.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI