Na Titus Mwombeki, KAGERA.
SERIKALI imeendelea kuwafuatilia kwa ukaribu Jumla ya watu 193 wakiwemo watumishi wa afya waliotangamaa na wagonjwa wa ugonjwa wa Marburg mkoani Kagera huku jitihada za kuanza kutoa huduma ya upimaji wa joto la mwili katika maeneo ya stendi za mabasi na bandalini likitarajiwa kuanza .
Hayo yamesemwa na mganga mkuu wa Serikali nchini Prof Tumain Nagu wakati akiongea na waandishi wa habari akielezea jinsi selikari kupitia wizara ya afya inavyozidi kupambana na ugonjwa huo.
"Hadi kufikia tarehe 23 mwezi Machi mwaka huu bado tuna jumla ya wagonjwa walioripotiwa nane na watano kati yao walifariki dunia watatu bado wanaendelea na matibabu na afya zao zinazidi kuimarika, bado visa havijaongezeka pia tunaendelea kuwafatilia watu waliotangamaa na hawa wagonjwa kwa mpaka sasa tuna jumla ya watu 193 ambao wametangamaa na wagonjwa wa Marburg na kati ya hao 89 ni watumishi wa afya na 104 wako kwenye jamii" alisema
Bi Nagu amsema kuwa serikali bado jitihada kubwa zinaendelea kufanyika ikiwa ni pamoja na kuzidi kuongeza wataalamu wa afya na kutoa elimu kwa wananchi ili kuhakikisha wananchi wanakuwa salama.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kuotoa taarifa katika vituo vya afya wanapoona mtu mwenye dalili za ugonjwa huo ili ikiwa ni mtu kuwa na homa,kitapika damu,kutokwa damunsehemu mbalimbali sehemu za mwili na figo kushindwa kufanya kazi.
Hamza kamugisha, mkazi wa mtaa wa Rwamishenye Manispaa ya Bukoba ameipongeza serikali kwa kuendelea kutoa hali ya ugonjwa huu kwani inawasaidia wananchi hao kuendelea kuona kasi ya ugonjwa huo nao kuendelea kuchukua hatua madhubu za kujikinga na ugonjwa huo.
0 Comments