Na Gift Mongi _ Moshi
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa fedha kiasi cha milioni 475 Kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya TPC - Samanga inayojengwa kwa kiwango cha changarawe jambo lililoelezwa kuwa ni suluhisho kwa wakazi wa eneo hilo.
Katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi huo mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ametembelea kata ya Arusha Chini katika kijiji cha Chemchem na kuzungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa kata hiyo na wananchi.
Aidha mbunge huyo kwa kushirikiana na diwani wa kata hiyo Leonard Waziri wameeleza miradi ya maendeleo iliyotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.
"Miradi iliyotekelezwa ni kwenye sekta za miundombinu ya barabara, afya, ujenzi wa madarasa na mikopo kwa akina mama na vijana"ameeleza Prof Ndakidemi
Mbunge amewaambia wananchi kuwa, kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita, serikali imetoa zaidi ya shillingi milioni 900 katikakKata ya Arusha Chini ili kutekeleza miradi ya maendeleo.
Aidha katika mkutano huo baadhi ya wananchi walimweleza mbunge kuwa kero yao kubwa ni kukosekana kwa daraja linalounganisha mto Ronga na kijiji cha Chemchem.
"Kero nyingine ni pamoja na kukosekana kwa shule ya sekondari katika vijiji vya Mikocheni na Chemchem ambapo wanafunzi hulazimika kutembea umbali wa kilomita 34 kufuata elimu"ameeleza Godhope Mshiu
Kero nyingine kubwa ni ile ya mafuriko ya mara kwa mara ambapo wananchi walimwomba mbunge awasemee wajengewe skimu ya umwagiliaji ili kuyatumia maji ya mto Ronga vizuri.
Viongozi hao kwa pamoja wamejadiliana na kukubaliana kubeba kero zilizojitokeza kwenye mkutano na wananchi.
Kuhusu kero ya ukosefu wa daraja katika mto Ronga, wameafikiana kuipeleka TARURA ambapo kuhusu ukosefu wa sekondari, mbunge na diwani wamesema watamwomba mkuu wa wilaya atoe idhini ya kujenga shule katika kijiji cha Mikocheni kwani eneo limeshapatikana.
Mbunge amewahimiza wananchi wachangie fedha na nguvukazi ili ujenzi uanze ambapo yeye na Diwani walitoa ahadi ya mifuko 200 ya saruji.
Kuhusu uhitaji wa skimu ya umwagiliaji, Mbunge amesema kwamba atawasilisha kero hiyo wizara ya kilimo ili miundombinu ya umwagiliaji ijengwe na baadaye iweze kuwafanya wakulima wazalishe mwaka mzima kwa tija.
Wakihitimisha ziara ya Mbunge, wenyeviti wa vijiji vya Mikocheni na Chemchem wamemshukuru Mbunge kwa kuwatembelea na kwa furaha wazee wa kijiji cha Chemchem
0 Comments