Header Ads Widget

MAKADA CCM WAZIDI KUMVAA LEMA

 




Na Gift Mongi MATUKIO DAIMA APP,MOSHI


Matamshi yaliyotolewa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema juu ya waendesha bodaboda kuwa ni kazi ya laana imeonekana kuwaibua baadhi ya makada wa chama cha mapinduzi (CCM)na kudai ni lugha za dharau juu ya kundi hilo.


Mbali na kauli hiyo Lema alienda mbali zaidi kuhusu vicoba na kusema kuwa ni umaskini na kuwa hata yeye amemkataza mkewe aisishiriki katika vikundi hivyo vya kuweka na kukopa.


Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima amesema kuwa lugha hizo hazifai na kuwa vijana hawatakiwi kufumbia macho maneno hayo ya dharau.


"Ndugu bodaboda njooni huku CCM kunafurahisha mno na kitendo cha Lema kutulaani bodaboda na kutuita maskini na kuwatukana mama zetu wa vicoba na kuwaita maskini wakati wengine sisi tumesoma kwa vicoba inasikitisha na tutamfurahisha dawa yake ipo jikoni"anaeleza Shirima


Shirima anasema kuwa kazi ya bodaboda ni huduma kama zilivyo nyingine na ni kazi halali kwani imechangia vijana wengi kuweza kujiajiri hali iliyowapelekea kuondokana na umaskini.


Anasema kuwa kauli hiyo sio nzuri kwa afya ya ustawi wa vijana ambapo wamekuwa wakiwekewa mazingira rafiki katika kujiajiri na kuwa ingefaa zaidi kama angekuja na suluhisho na nini kifanyike.


Martin Kiwelu dereva wa bodaboda katika maeneo ya Njiapanda wilayani Moshi amesema kuwa kauli hiyo imewastaajabisha na kuwa wamekuwa wakitoa huduma hiyo ambayo pia inaweza kukidhi mahitaji yao ya kila siku.


"Sisi tunaendesha hizi bodaboda lakini maisha yanaenda tunatimiza majukumu kama walivyo wafanyakazi wengine ila kusema ni laana kiukweli hajatutendea haki hata kidogo"anasema


Maurine Mtey mkazi wa manspaa ya Moshi anasema vicoba vimewawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuwa wameweza kufanya mambo ya maendeleo kama kumilimi nyumba na hata kusomesha watoto.


"Vicoba vinatusaidia sana katika kupiga hatua za kiuchumi ila bila vicoba vitu vingi tusingeviweza maana hatuna sifa za kukopesheka benki"anasema


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI