Header Ads Widget

ILANI YA CCM YALETA FARAJA KIBOSHO KINDI

 


Na Gift Mongi,MATUKIO DAIMA APP

MOSHI


Katika kuhakikisha ufaulu unaongezeka sanjari na kutatua kero mbalimbali katika jamii mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi ametembelea baadhi ya taasisi zilizopo katika kata ya Kibosho KINDI na kujionea Hali ya uendeshwaji wake.


Katika ziara inayoendelea katika kata hiyo Prof Ndakidemi pia ameambatana  na  viongozi wa kata wa chama cha Mapinduzi na wale wa serikali wakiwa na diwani mwenyeji  Samwel  Kirumbuyo.


Viongozi hao wamekagua miradi ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Chewe na Zahanati zinazopatikana katika kata hiyo.



Katika ziara hiyo pia wamekagua majengo mbalimbali ya shule kama vile jengo la Uutawala,  maabara za kisasa za fizikia, biolojia na kemia, chumba Cha kisasa cha Tehama, Madarasa, jengo la maktaba pamoja na jiko la kisasa. 


Aidha akisoma risala mkuu wa shule hiyo Mwl.  Thomas Bombo ameeleza kuwa pamoja na mafanikio hayo bado shule inakabiliwa na changamoto mbalimbali


Ukosefu wa mashine ya kurudufu(Photocopy)mashine na kompyuta kwa ajili ya matumizi ya ofisi na kudurufisha mitihani,   Ukosefu wa vifaa vya Michezo jezi na mipira Ukosefu wa walimu wa somo la hisabati upungufu vitabu vya ziada na  Ukosefu wa vifaa vya maabara  kwa ajili ya kufanyia mafunzo kwa vitendo. 



Viongozi hao pia wamekagua mradi wa zahanati ya Chekereni, ambapo kwa sasa mradi huo umekamilika. 


Baada ya kukagua miradi hiyo miwili, mbunge na viongozi wengine walipata nafasi ya kuotesha miti ya kivuli kama alama ya kumbukumbu kwa shule hiyo. 


Akiongea na wanafunzi, waalimu na wazazi, mbunge amewaambia kuwa amezipokea changamoto zao, na atazifikisha kwenye mamlaka husika. 



Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya CCM tawi la Chekereni-Weruweru,   na Diwani waliwakilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha miaka miwili kwenye uongozi wao. 


Pia wameeleza kuwa kwa kipindi hicho kifupi, serikali imetekeleza  miradi mbali mbali katika sekta za afya, elimu, barabara, maji na maendeleo ya jamii yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.9.


 Katika miradi hiyo,  ripoti ilionyesha kwamba vikundi vilivyonufaika na mikopo ya Halmashauri ni vingi na wanaendelea kuomba.


Wananchi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara  wameeleza kero zao ambapo  kero kubwa ni kukosekana kituo cha polisi katika kijiji cha Chekereni Weruweru. 



Akijibu kero hizo, Prof Ndakidemi amewaambia wananchi wajipange watafute eneo na kwa kutumia michango waanze ujenzi wa kituo hicho kwani naye ataunga mkono kama mdau. Alisema, swala la ubovu wa barabara linafanyiwa kazina TARURA. 


Katika mkutano huo mbunge ametoa mchango wa kiasi cha shilingi  laki tano kama msaada wa kununua sare kwali walimwambia kuwa walikuwa na changamoto hiyo.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI