Na Zulfa Alfani Matukio Daima App Simiyu
Waziri Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 duniani zenye maambukizi makubwa ya kifua kikuu ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 87 ya wagonjwa wote duniani.
Waziri mkuu Majaliwa ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Simiyu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo waziri ya afya Ummy Mwalimu amesema watu 25,800 nchini hufariki dunia kila mwaka kutokana na kifua kikuu ambao ni sawa na watu 71 kila siku huku akiongeza kuwa serikali imejitahidi kuhakikisha vipimo na dawa zinapatikana katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini.
Awali akitoa salamu za mkoa wa Simiyu mkuu wa mkoa huo Dkt Yahaya Nawanda amesema mkoa huo umepokea mashine nane za kupima vinasaba vya vimelea vya kifua kikuu.
Serikali kwa kushirikiana na wadau nchini iliweza kutumia wahudumu wa afya ngazi za jamii wapatao 3600 kutoa elimu kwa wamiliki wa maduka ya dawa muhimu 1440 na waganga wa tiba asili 900 ili waweze kutoa elimu na vifaa kwa wahisiwa wa kifua kikuu ili waende kwenye vituo vya kutolea huduma.
0 Comments