Header Ads Widget

LINDI YAKADIRIWA KUWA TAKRIBAN WATU 10,250 WASIOONA

 



Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


MGANGA Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Dkt Alex Makalla amesema Mkoa huo unakadiriwa kuwa takriban watu 10,250 wasioona na watu 41,000 wenywe upungufu wa kuona wakati na wa kiwango cha juu .


Akiongea leo Jijini Dodoma kwenye uzinduzi wa Miradi wa afya ya macho kwa ufadhili wa shirika la Christoffel Blinden Mission shirika lilitoa Shilingi za kitanzania  819 ,238,062  zinazoenda kutekeleza mradi wa Toshelezi na jumuishi za afya ya macho kwenye Mkoa wa Lindi kwa Miaka minne.


Dkt Makalla amesema lengo kuu la mradi ni kuongeza juhudi za kupunguza upungufu wa kuona unazuilika na kujumuisha huduma msingi na jamii ya Afya ya macho na kuimarisha Vitengo vya huduma za macho kwa ajili ya utolewaji wa huduma jumuishi za afya ya macho katika  Mkoa wa Lindi .



Amesema Huduma za macho kwa mkoa wa Lindi zimekuwa zikitolewa Katika Hospitali hiyo ya Lindi ya Rufaa ya Sokoine na Hospitali mbili za Wilaya (Ruangwa na Nachingwea) Kati ya Halmashauri 6.


"Hata hivyo huduma zinazotolewa kwenye Hospitali za Wilaya ni huduma msingi kwani Kuna uhaba wa Watumishi (Watumishi waliopo ni wauguzi wa fani ya macho tu) na miundombinu kwa ajili ya Huduma za macho," 


Huku aliongeza Kusema " Hospitali za Halmashauri za Wilaya ya Kilwa,Mtama,Liwale na Lindi Manispaa hazina wataalamu wa huduma za macho kwa ajili ya Kutoa huduma kwani wataalamu waliopo walipata mafunzo ya miezi mitatu tu,"amesema Dkt Makalla


Hata hivyo amesema mkoa mzima wa Lindi kwa mwaka 2022,ni Watu 8,805  tuwaliofika kwenye vituo vya tiba Kati ya Watu 205,000 waliotakiwa kuonwa kila mwaka kulingana na makadirio ya ukubwa wa matatizo ya macho ambapo Kati ya hai asilimia 10 walikuwa hawaoni kabisa na asilimia 24.6 walikuwa na upungufu wa kuona inayofanya asilimia ya wenye upungufu wa uoni kuwa 34.6



Naye Dkt Bernadetha Shilio Meneja Mpango wa Taifa wa huduma za macho aliomba uimarishaji wa huduma Toshelezi ya Afya ya macho .


Amesema mradi huo wenye thamani ya Shilingi za kitanzania 646,850,800, una lengo kuu la kuongezeka uwezo Mpango wa Taifa wa huduma za macho na kuuwezesha kuratibu ushirikiano wa wadau wote ili kukuza Utoaji wa huduma jumuishi za macho, zinazojitosheleza na zenye ubora hapa nchi. 


Kwa Upande wake Muuguzi Mkuu wa serikalli  Ziada Sella akiongea kwa niaba ya katibu Mkuu wizara ya Afya Seif Shekalaghe Amesema jicho ndio kiungo muhimu kwa binadamu ni wajibu huduma za afya ya macho zinakinga kuzuia upungufu wa kuona ambapo Takwimu kutoka shirika la afya Duniani WHO zinasema asilimia 1ya Watu kwenye nchi zinazoendelea na za uchumi wa Kati wanaulemavu wa kuona unakadiriwa kuwa watanzania 620,000 hawaoni.


Amesema Takwimu za hapa Tanzania zinaonyesha Watu Milioni 1,347,000 tu kwa mwama 2022 ndio waliofikiwa na huduma za macho katika vituo vya kutolea huduma za afya ya macho ikilinganishwa na uhitaji wa takriban watu milion 12 ,400,000 na Kati yao asilimia 33.5 wanakuwa tayari wana upungufu wa kuona ikijumuisha ulemavu wakutokuona.



Sambamba na hilo Muuguzi Mkuu huyo Amesema matatizo ya macho yalioongoza kwa mwaka 2022 yalikuwa Ni upeo Mdogo wa macho ,kuona unaoorekebishika kwa miwani ,uvimbe kwenye ngozi nyororo ya jicho ,Mtoto wa jicho, Shinikizo la damu na matatizo kwenye retina


Naye Mkurugenzi Mkazi CBM Nchini Tanzania Nadia Mahenge Amesema shirika hilo limeundwa Miaka 110 iliyopita na wamekuwa wakifanya na nchi 50 duniani ikiwemo na Tanzania kwa kufanya shughuli mbalimbali ambapo mwaka huu shirika hilo limetoka fedha kwenye afya ya macho.


"Ni ukweli usiopingika bila kuwa na macho mazuri yenye kuona huwezi kufanya shughuli yoyote ya Maendeleo hivyo tumeona Kinga Bora kuliko tiba hivyo wanaimani mradi huo unakuja kuleta matokeo chanya kwa Wananchi kupimwa na kupatiwa huduma mapema ya macho Kabla ya kuwa walemavu wa macho hivyo tufanye kazi Kama Timu ili kuleta tija .



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI