Header Ads Widget

KATIBU MKUU KILIMO AWAPONGEZA VIJANA WALIOJITOKEZA KWENYE FURSA ZA KILIMO BBT

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma


NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dk Hussein Omar  amesema kuwa Wizara ilipotangaza nafasi kwa vijana wanaotaka kuingia kwenye fursa za kilimo vijana wengi walijitokeza jambo ambalo ni jema na limeonesha ni kwa jinsi gani vijana wana kiu na fursa zulizopo kwenye kilimo.


Aliyasema hayo  Katika mkutano wa utekelezaji wa Programu ya Vijana ya Building  Better Tomorrow, Wizara ya Kilimo na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali yanayofanya kazi na vijana katika sekta ya kilimo.


Amesema wizara inashirikiana na wadau wote muhimu katika utekelezaji ili kuhakikisha rasilimali zinazotumika 


katika kuwezesha vijana kushiriki katika kilimo zinatumika kwa tija na ufanisi kwa mustakabali wa ukuaji wa uchumi.


“Katika program ya BBT Vijana walijitokeza wa kutosha na waliochaguliwa ni 812 ambao ni asilimia nne tu ya vijana 20.000 walioomba mafasi hizo, hii inaonesha ni kiasi gani vijana wana kiu na fursa kubwa iliyopo kwenye kilimo, alisema


Alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizopo, sekta ya Kilimo inachangia asilimia 26 ya Pato la Taifa (GPD) wakati huo zaidi ya ajira 65 zinategemea sekta ya kilimo.


Amesema kuwa Tanzania ina NGOs zaidi  ya 4,000 zinazojihusisha na sekta ya kilimo isipokuwa uwekezaji haujaweza kuratibiwa ipasavyo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya NGOs kutokutoa taarifa sahihi kuhusu shughuli zao.


 Aidha amesema utafiti unaonesha kati ya NGOs 10 zinazojihusisha na kuwawezesha vijana kushiriki katika sekta ya kilimo, NGOs 8 zimejikita katika masuala ya uhamasishaji.


Alisema kuwa katika utekelezaji wa BBT, mpango ni kufanya kazi kwa kushirikiana na wadau wote muhimu ikiwemo NGO.


"Mkutano huu unajadili na kuona namna ya kuimarisha ushirikiano wa Wizara ya Kilimo (Serikali) na NGOs katika utekelezaji wa miradi ya kuwawezesha vijana na wanawake kufanya kilimo biashara chini ya programu ya BBT," amesema


Hata hivyo amesema kuwa Wizara imekamilisha uchambuzi wa maombi yaliyowasilishwa na vijana. 


"Utekelezaji wa BBT utaanza na vijana 812 kwa awamu ya kwanza, kati yao wasichana ni 282 sawa na asilimia 23.34na wavulana ni 530 sawa na  asilimia 76.65 Vijana waliochaguliwa ni asilimia nne ya vijana 20,227 walioomba kupata fursa ya kujifunza na kufanya kilimo biashara," amesema 


kwa upande wake, Mratibu Miradi wa BBT, Vumilia  Zikankuba alisema kuwa mpango mkakati wa program ni uanzishwaji wa maeneo maalum kwa ajili ya vijana waliopo katika kilimo biashara ili kuwezesha upatikanaji wa ardhi ya kilimo kwa vijana.


Amesema uanzishwaji wa maeneo yatakayoboreshwa na miunsombbunu na kugawanywa kwenye mashamba vitalu.


Pia amezitaka sekta binafsi nchini kutengeneza fursa za vijana kwenye kilimo.


Alisema kuwa matokeo ya sensa ya watu na makazi 2022 yamebainisha kuwa, zaidi ya asilimia 44 ya watanzania ni vijana na wastani wa umri kwa Watanzania wote ni miaka 18. 


“Nchi yetu ni ya Vijana ambapo wengi hawana ajira licha ya kuwepo kwa fursa mbalimbali kwenye sekta ya Kilimo katika mnyororo wa thamani., alisema


Alisema kuwa kuna wajibu mkubwa wa kutengeneza fursa za ajira kwa vijana na Mashirika yasito ya kiserikali (NGOs)yana nafasi kubwa zaidi.


Alisema kuwa tija katika uzalishaji ni wastani wa tani 1.8 kwa ekari ikilinganishwa uwezekano wa kufikia tani 8 kwa mazao ya nafaka. 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI