Header Ads Widget

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE NA UWEKEZAJI YAAGIZA TRC KUSIMAMIA UJENZI WA SGR MWANZA - ISAKA KWA UKARIBU.

 


Kamati ya Kudumu ya Bunge  Uwekezaji, Mitaji ya Umma ( PCI ) imeliagiza Shirika la Reli Tanzania ( TRC ) kusimamia hatua zote za ujenzi wa mradi wa reli ya kisasa ya mwendo kasi kipande cha tano ( SGR ) Mwanza – Isaka kilometa 342 uweze kukamilika kwa wakati.



Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Jerry Silaa baada ya kutembelea na kukagua ujenzi huo katika maeneo tofauti tofauti inapojengwa reli hiyo mkoani ambapo ujenzi wa reli hiyo umefikia asilimia 28 tangu ulipoanza kutekelezwa mwaka 2021.



Ujenzi wa reli kipande cha tano, Mwanza – Isaka utagharimu kiasi cha shilingi tilioni 3.06 hadi kukamilika kwake huku mkandarasi akiwa tayari ameishalipwa zaidi ya shingi bilioni mia saba na unatarajiwa kukamilika mwezi Februari 2024.



Meneja  Mradi wa  SGR Mwanza – Isaka Christopher Kalisti amesema, kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa tuta ambao umefikia asilimia 58 na ujenzi wa madaraja umefikia asilimia 47 ikiwemo utandikaji wa reli umefikia kilometa nne na nusu sambamba na mfumo wa masiliano.



Kamati hiyo imempongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajli ya utekelezaji wake.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI