Mahakama katika mji wa Malegaon katika jimbo la Maharashtra nchini India imemuamuru mshtakiwa kusali mara tano kwa siku kwa siku 21 zijazo ili kumuadhibu kwa kupigana.
Uamuzi wa Jaji Tejwant Singh Sindhu pia uliamuru mshtakiwa mwenye umri wa miaka 30 Rauf Umar Khan kupanda miti miwili karibu na msikiti ili kumwondolea kesi hiyo ya uhalifu wake na kutunza miti hiyo miwili.
Hakimu alimpata mwanamume huyu na hatia ya kumjeruhi mwenzake katika mgogoro wa mtaani.
Hakimu huyo pia alimuamuru afisa kilimo wa wilaya hiyo kufuatilia utekelezaji wa amri ya mahakama na kumruhusu kutumia jeshi la polisi ikibidi kutekeleza agizo hilo.
0 Comments