Na Gift Mongi MATUKIODAIMA App,Moshi
Tunaweza kusema kuwa bado shamrashamra za maadhimisho ya siku ya wanawake duniani zinaendelea ambapo mambo mbali mbali yamefanyika kuonyesha utofauti wa siku hii muhimu Kwa akina mama.
Kama ambavyo imekuwa ni desturi kwao kufanya maadhimisho haya mwaka huu huenda yamekuwa yakipekee zaidi ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.
Utofauti wenyewe ni kuwa karibia kila sehemu ambapo maadhimisho yamefanyika wamekuja na njia mpya katika kuonyesha jamii kuwa kweli ni jeshi kubwa na kuwa wanawake wanaweza.
Katika kuadhimisha siku hiyo mbunge wa viti maalum mkoa wa Kilimanjaro Ester Maleko naye akaungana na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Ashira Girls kwa kutoa msaada wa vifaa mbalimbali.
Mbunge huyo ameweza kugawa taulo za kike Kwa wanafunzi hao lakini pia kutoa mchango wake katika kuhakikisha kunapatikana madawati ya kutosha kwenye shule hiyo
"Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani tumetembelea wanafunzi Ashira Girls nikiwa na mwenyekiti wetu na wajumbe wa baraza Moshi vijijini nimekabidhi ahadi yangu fedha za madawati 1.6 mil na kugawa taulo za kike kwa wanafunzi 781"anasema Ester
Anasema kutoa mchango huo ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa na ameona ni vyema kwenda mbali zaidi katika kutoa msaada huo kwa wanafunzi hao ambao ndio viongozi watarajiwa
Baadhi ya wakazi wa kata ya Marangu Mashariki wameeleza mapokeo ya zawadi hizo na kuwa inachangia katika kukuza sekta ya elimu na ni wajibu wa kila mwananchi kujitoa katika kuchanga kadri ya uwezo wake.
Deliphina Mtui anasema suala la kuchangia katika sekta ya elimu sio jukumu la serikali pekee bali hata kwa mdau mmoja mmoja kama alivyofanya mbunge huyo.
"Lazima na sisi tuhakikishe kwa hata kidogo tulichonacho tunashiriki kuchangia ukuani wa elimu kama alivyofanya mbunge badala ya kubaki na dhana kuwa serikali itatekeleza kila jambo"anasema









0 Comments