Header Ads Widget

DC ZAINABU ABDALLAH ATOA MAAGIZO MAZITO PANGANI.

 


NA,AMINA SAID,TANGA


Mkuu Wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainabu Abdallah amewataka wakuu wa Idara, Taasisi pamoja na Mkurugenzi wilayani hapo kushirikiana pamoja na Madiwani katika Vikao vya mapato na matumizi ili kudhibiti Taarifa zisizo sahihi kutoka kwa wataalamu pindi wanapokuwa katika maeneo yao


Mh Zainabu ametoa Maagizo hayo kwenye Kikao Kazi cha kujadili miradi ya maendeleo katika wilaya ya hiyo kilichowakutanisha wakuu wa Idara, vitengo na Taasisi pamoja na Madiwani na kusema kupitia vikao, Madiwani wataweza kutoa Taarifa sahihi ya mazingira yaliyopo katika maeneo yao pamoja na kukagua vyanzo mbalimbali ili kuhakikisha wanafikia malengo ya ukusanyaji wa mapato ifikapo mwezi June mwaka huu.


Amesema kipaumbele cha pili katika Wilaya hiyo ni usimamizi wa Miradi ya Maendeleo ambapo kumekuwa na Changamoto ya Utekelezwaji wa miradi kwa wakati na wakati mwingine miradi kujengwa chini ya kiwango, hivyo kupitia vikao vya kila mwezi watafanya Tathmini ya Mradi mmoja baada ya mwingine katika hatua za Utekelezaji, Changamoto pamoja na mafanikio ya miradi hiyo.


Aidha Mhe Zainabu amewataka wataalamu wa Idara na Taasisi kuwahusisha viongozi kuanzia ngazi ya Wilaya kuhusu Mradi wowote kabla haujatekelezwa ili wapate Taarifa na kuujua kwa kina juu ya Mradi huo ambapo amesema kumekuwa na Changamoto ya miradi kutelekezwa bila kiongozi yoyote kushirikishwa hivyo kupitia ushirikishwaji wataweza kushirikiana kwa pamoja ili kumaliza Mradi kwa wakati.



Pia amewataka Wakuu wa Idara, na Taasisi kuacha tabia ya kukaa ofisini na kuwatuma Maafisa kata katika kutatua kero za wananchi, kwani na wao wanawajibu wa kwenda kutatua kero hizo ambapo ameahidi kutembelea vijiji vyote 33 ili kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani hapo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI