Bodi ya Ushauri na Utawala wa Wakala ya Usajili Biashara na Leseni ( BRELA ) imetoa mafunzo kuhusu Dhana ya wamiliki manufaa wa kwenye Makampuni kwa Mamlaka zilizokasimiwa lengo likiwa ni kuwaelimisha kuhusu marekebisho na maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha wanatoa huduma bora za utendaji wao wa kisheria kila siku
Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika Ukumbi wa Victoria Palace Hotel Jijini Mwanza ambapo yamewashirikisha washiriki kutoka ofisi ya Takukuru Mkoa wa Mwanza , Ofisi ya Mwendesha Mashitaka, Ofisi ya Makosa ya Jinai,Idara ya Uhamiaji pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa Mwanza
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara Brela Meinrad Rweyemamu amesema, Lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo kwa ajili ya uchunguzi na uendeshaji wa mashitaka ya jinai yanayohusu makampuni mbalimbali yanaoyafanya biashara hapa nchini.
Kimsingi ndiyo wamepewa mamlaka kisheria kupata taarifa mbalimbali kutoka katika makampuni yanayofanya biashara na wananchi hapa nchini na leo tumeamua kuwakutanisha kwa ajili ya kuwapatia mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kampuni na Majina ya Biashara Brela Meinrad Rweyemamu.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza Bodi ya Ushauri na Utawala ya Usajili Biashara na Leseni kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uwezo na uelewa mpana katika suala marekebisho na maboresho mbalimbali ya kisheria na kimfumo
0 Comments