Header Ads Widget

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR AAHIDI KUTATUA KERO YA UHAMISHO KWA WANAFUNZI TOKA ZANZIBAR KWENDA TANZANIA BARA.

 



Na Mbaruku Yusuph Matukio Daima APP Tanga. 


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Lela Mussa ameahidi kushughulikia tatizo linalowakumba wanafunzi wanaohama toka Zanzibar kwenda Tanzania Bara na wale wanaotoka Bara kwenda Zanzibar kwa kile kinachodaiwa lazima wanafunzi hao wapate barua toka kwa Kamishna wa Elimu Mkoani Dodoma.


Hayo ameyabainisha wakati wa Maadhimisho ya kumbukizi ya kuzaliwa mwanzilishi wa Chama cha Skauti Duniani Sir Baden Powel yaliyofanyika Kitaifa Jijini Tanga na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za kiserikali.



Waziri Mussa alisema ni kweli kumekuwepo na kesi zinazohusiana na wanafunzi hao wanapotoka sehemu moja kwenda nyingine hukosa barua zitakazowaruhusu kuendelea na masomo jambo ambalo linapaswa kushughulikiwa na Mawaziri wa sekta hiyo ya Elimu toka pande zote mbili.


Aidha alisema uwepo wa mfumo wa online kwa ajili ya  kushugulikia barua za uhamisho wa wanafunzi hao toka Bara kwenda Visiwani au wanaotoka Visiwani kwenda Bara utawarahisishia wazazi ambao wanashindwa kufika Dodoma kwa Kamisha wa elimu kupata barua hizo na kuzituma katika ofisi zinazostahili.


Mbali na hayo Waziri Lela ambae pia ni Makamu wa Rais wa Chama cha Skauti Tanzania alizungumzia maadhimisho hayo ya Skauti na kusema kuwa ipo haja ya Serikali zote zitambue umuhimu wa Chama hicho kwa kujua kuwa ndio hazina ya baadae kwa Taifa zima.


Aidha alisema chama hicho lazima kijenge mshikamano kuanzia ngazi za Wilaya hadi Taifa na kujenga misingi imara yauwelewa,uzalendo,maadili bora na uwadilifu ili kiweze kuwa mstari wa mbele kupinga udhalilishaji kwa jamii.



Hata hivyo alimuomba Kamishna mpya wa Skauti Nchini Rashidi kupambana na kunusuru vitendo hatarishi vinavyofanywa katika jamii na kutambua Sheria zilizopo zinambana aliyetenda vitendo vya udhalilishaji huku aliyedhalilishwa akibakiwa na maumivu.


"Hizi sheria kweli zinambana mdhalilishaji lakini aliyefanyiwa vitendo viovu anabakia na maumivu kwa maana hiyo Kinga ni bora kuliko tiba"Alisema Waziri Mussa.


Aliwataka maskauti hao kuwa mfano mzuri wa kimaadili na kupinga vitendo vya udhalilishaji wa watoto na  jamii kwa ujumla sambamba na walimu wawe mstari wa mbele na kukemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya walimu kinyume na taratibu zao za kazi.


Kwa upande wake Naibu Kamisha Mkuu wa Skauti Tanzania Abubakar Mtiti alisema watazingatia kauli mbiu ya Chama hicho ambayo inasema "msingi na umoja wetu ndio nguzo ya Skauti endelevu Tanzania" 


Alitoa rai kwa jamii kujiepusha matumizi ya plastiki na kufanya hivyo kutaipelekea Duania kuwa salama huku akiwaagiza Skauti wote waliohudhuria katika maadhimisho hayo  wanahakikisha wanapanda miti ya matunda au kivuli katika maeneo yao wanayoishi au mashuleni ili kuepukana na mabadiliko ya hali ya Nchi.


Awali akitoa salamu za Mkoa Tanga Afisa Elimu Mkoa Newaho Mkisi alisema ushirikiano uliopo baina ya Tanga na Zanzibar hautakuwa na Tija kama hakutashughulikiwa tatizo la uhamisho wa wanafunzi toka Tanga-Zanzibar au Zanzibar-Tanga jambo linawakwamisha wanafunzi wengi na kupelekea kati yao kushindwa kuendelea na masomo.



Mkisi ambae alimuakilisha Katibu Tawala Mkoa huku akisoma taarifa ya Mkuu wa Mkoa Tanga alisema kuwa wanafunzi wa madarasa ya mitihani ambao wengi wao hawajasajiliwa ni kutoka Zanzibar ambao kuna changamoto ya kupata barua ambayo lazima ifuatwe Dodoma kwa Kamishna wa elimu.


Aidha alisema ipo haja kwa Mawaziri wa elimu toka pande mbili Zanzibar na Tanzania Bara watafute ufumbuzi wa changamoto hiyo kwa kutuma barua kwa njia ya online badala ya mfumo wa sasa ambao sio rafiki. 


  

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI