Na Amon Mtega,Mbinga.
BAADHI ya Wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho ipasavyo kwa kuwaletea maendeleo Wananchi.
Akizungumza mwenyekiti wa Wazee Wilaya ya Mbinga Osmund Kapinga kwenye ukumbi wa CCM wa Wilaya hiyo waliokuwa wamealikwa na katibu wa CCM Wilaya hiyo Mary Mwenisongole kwa lengo la kuwatambua wazee na kuwashukuru kwa kuendelea kukilinda Chama hicho hadi sasa kimetimiza miaka 46.
Mwenyekiti Kapinga amesema kuwa Chama hicho kupitia mwenyekiti wake wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ilani ya Chama imeweza kusimamiwa vizuri hasa kwa kutekeleza miradi mbalimbali iliyopo kwenye ilani.
Kapinga amesema kuwa wao kama wazee wataendelea kukilinda Chama hicho kikamilifu ili kizidi kuwaletea maendeleo Wananchi wake na hatimaye Taifa lizidi kusongambele.
Kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya ya Mbinga Mary Mwenisongole akiwashukuru wazee hao amesema Chama Wilayani humo kinatambua mchango wa Wazee hao na kuwa amewaomba kuendelea kushirikiana ili Chama kizidi kushika dola pamoja na kuwasii baadhi ya Vijana waachane na tabia ya kujihusisha na vitendo viovu.
Katibu Mwenisongole licha ya kuwashukuru Wazee hao hadi sasa Chama kutimiza miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM lakini bado ametumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Wazee hao kwa kuwa tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo katika kipindi cha hivi karibuni hakupata nafasi ya kukutana na Wazee hao.
Aidha Wazee hao wameweka kumbukumbu ya kupanda miti katika eneo la Ujenzi wa ofisi mpya ya Chama hicho ngazi ya Wilaya ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa kutimiza miaka 46 ya CCM.
0 Comments