MRADI wa Youth Angency Mufindi (YAM) umeanza utoaji wa elimu ya Saikolojia Kwa vijana chini ya miaka 25 wanaotoka Katika mazingira Magumu kata tatu za wilaya ya Mufindi kuwawezesha kukabiliana na tatizo la msongo wa mawazo na Sonona
Mafunzo hayo ya siku 10 yameanza kutolewa jana Katika Ukumbi wa Yatima Igoda wilayani Mufindi Kwa kuunganisha vijana 100 toka vijiji 16 vya Kata ya Ihanu ,Mdabulo na Luhunga .
Akizungumza na vijana hao wakati wa Ufunguzi wa mafunzo hayo ,Mwenyekiti wa chama cha Watoa huduma za kisaikolojia Tanzania Dr Heriel Mfangavo alisema mafunzo hayo ni fursa kubwa Kwa vijana hao Kuelekea kujitambua na Kuondokana na mawazo mgando ya kutopiga hatua ya kimaendeleo na kuwa na mawazo ya kusonga mbele .
Alisema kuwa vijana hao ni wadogo kama hahatapatiwa tiba ya saikolojia mapema tatizo hilo wanakuwa nao na ukubwani wanaweza kufanya majanga makubwa yakiwemo ya mauwaji au kujiua .
Kwani alisema mfano mabinti waliopata mimba utotoni Kwa kubakwa ama kurubuniwa Hali hiyo huwa haifutiki kirahisi kwenye akili zao hivyo lazima elimu ya saikolojia iwapitie mapema ili wasiendelee kuteseka ama kutesa watoto .
Mbali ya mabinti pia alisema vijana walionyanyasika Kwenye familia Kwa kutelekezwa na baba mzazi wakiwa wadogo ama kupokonywa mali huwa wanakuwa na visasi hadi ukubwani.
Pia alisema kundi jingine linalohitaji msaada wa kisaikolojia ni kundi la watu wenye ulemavu ambao baadhi yao wanaishi na msongo wa mawazo na Sonona kutokana na vile walivyo .
Hivyo alisema wanasihi watakaofanya kazi katika mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kubaini changamoto zinazosababisha tatizo la msongo wa mawazo Kwa jamii ya watu wenye ulemavu na kuitafutia ufumbuzi
Alisema kutokana na ukubwa wa tatizo kwa vijana hao na watu wenye ulamavu mafunzo hayo yatakuwa na faida kubwa kwao na kuondokana na utegemezi .
Alisema kuwa mradi huo wa YAM ni mkombozi mkubwa kwa jamii ya wana Mufindi hasa maeneo ambayo yanazungukwa na mradi huo kwani utasaidia jamii yenye uhitaji kuishi kwa furaha zaidi .
Hivyo alisema suala la ulemavu linapelekea watu wengi kuishi kwa misongo ya mawazo na hata kupata matatizo mengine ya kiakili .
Dkt Mfungamo alisema baadhi ya mambo yamekuwa chanzo cha jamii kukutwa na msongo wa mawazo kama kukataliwa ,kutengwa na unanyapaa wa kimahusiano .
Pia alisema hali duni ya kiuchumi inapelekea watu kupata msongo wa mawazo hivyo kupitia mafunzo hayo yanayotolewa ni wazi jamii itakwenda kupunguza tatizo la msongo wa mawazo na hata kuweze kufanya shughuli kifanisi zaidi.
Kwa upande wao vijana wanaotoka Katika familia duni waliokatisha masomo kutokana na changamoto mbali mbali ikiwemo ya mimba Kwa mabinti wamepongeza mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) kwa kuwafikia kuwapa mafunzo ya Afya ya akili na msaada wa kisaikolojia .
Washiriki wa mafunzo hayo Agnes Kihongole mkazi wa Kanig'ombe akizungumza Kwa niaba ya wenzake alisema walifikia hatua ya kukata tamaa ya maisha baada ya kukosa fursa za elimu .
Kwani alisema Kwa upande wake hakubahatika kuendelea na Masomo ya Sekondari kutokana na wazazi wake kukosa ada.
Hivyo alisema kupitia mafunzo hayo ambayo ni mwanzo kwao kujitambua na pindi watakapojitambua ni rahisi kwao kufanya shughuli za kiuchumi.
"Tunaamini kupitia mafunzo haya tumepata ukombozi Katika maisha yetu na familia tunazotoka maana bila kujitambua ni vigumu kubaini nini Cha kufanya"
Pia alisema matarajio yake na wenzake ni kupewa nguvu ya uwezeshwaji ili kutimiza ndoto yao hiyo .
Akizungumza Kwa niaba ya Meneja mradi wa Yam Danford Mkumbo ambae ni afisa mradi huo alisema mradi huo ni WA Miaka minne unatekelezwa na Halmashauri ya Mufindi Kwa kushirikiana na mradi wa Foxes Community and wildlife conservation(FCWC) kupitia mradi wa YAM chini ya ufadhili wa Serikali ya watu Finland utakelekelezwa kwenye utanufaisha vijana na watoto wanaotoka katika familia duni zaidi ya vijana 770 atika vijiji 16.
0 Comments