Header Ads Widget

UWEZO WA UZALISHAJI WA UMEME NCHI NI MEGAWATI 1,820





Na Hamida Ramadhan Matukio Daima APP Dodoma

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema uwezo wa uzalishaji wa umeme nchini ni Megawati 1,820, kwa sasa mitambo iliyopo inazalisha Megawati 1,300.


Mkurugenzi Mtendaji kutoka Shirika hilo la TANESCO Martin Mwambene aliyasema hayo leo jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na utekelezaji wa taasisi hiyo.


Mwambene amesema Shirika hilo linafanya miradi kadhaa ambayo inasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka ambapo malengo ni kufikia Megawati 5,000 ifikapo mwaka 2025.


Amesema Mradi wa Umeme wa bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88 ambapo sasa hivi tumeanza kujaza maji ambayo kwa sasa yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.


"Shirika la TANESCO lina miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ikiwemo ya gesi na jua, pia kuna vyanzo binafsi vyenye uwezo wa kuzalisha umeme mfano viwanda vya sukari," Amesema 



Na kuongeza Kusema"Miradi  ya uzalishaji umeme inaenda sambamba na miradi ya kusafirisha umeme, katika mradi wa JNHPP kuna njia ya kusafirisha umeme itakayoanzia Rufiji mpaka Chalinze na tayari transfoma kubwa takriban sita zimepelekwa zinasubiri kufungwa," Amesema Mwambene.


Aidha Amesema kuna baadhi ya mikoa ikiwemo Rukwa na Katavi haipo katika Gridi ya Taifa, hivyo kuna laini ambazo zitajengwa ambazo zitakuwa zinaunganisha nchi na nchi nyingine ambapo karibu nchi nzima itakuwa ipo katika mfumo wa Gridi ya Taifa.


Amesema Mradi wa Gridi Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6,000, mita laki 7 za umeme, nguzo 380,000, ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa KM 40,000, ujenzi wa vituo 14 vya kupoza umeme na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takriban KM 948.


"Mradi huu wa Gridi Imara ni ushahidi kwamba matatizo ya umeme yaliyopo nchini tunayafahamu na tunatarajia mradi huu utayatatua," amesema


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI