Wananchi visiwani Zanzibar wametakiwa kuendelea kudumumisha Umoja na mshikamano sambamba na kumuunga mkono Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuifungua Zanzibar kwa kupiga hatua za maendeleo.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk. Khalid Salum Mohamed ametoa wito huo wakati akizungumza na viongozi wa kampuni ya ujenzi ya HASSAN ALLAM kutoka nchini Misri waliofika Afisani kwake Kisauni kwa ajili mazungumzo yaliohusika na ushirikiano katika kutekeleza miradi ya miundombinu.
Mhe. Waziri amesema kuwa ipo haja kwa wananchi kuendelea kudumumisha hali ya ushirikiano na usalama ili kuwavutia zaidi wawekezaji pamoja na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuifungua Zanzibar kiuchumi.
Katika mazungumzo hayo Waziri Dk. Khalid ameeleza kwamba, kampuni hiyo imeonesha nia ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya miundombinu ikiwemo barabara, bandari pamoja na miuondombinu ya viwanja vya ndege.
“Chini ya uongozi wa Rais wetu Dk. Hussein Ali Mwinyi makampuni mengi yamehamasika kuja Zanzibar kutaka kuekeza na kushiriki katika ujenzi wa miundombinu kutokana na mazingira mazuri yaliojengeka” Alisema Waziri Dk. Khalid
Mhe. Waziri amefafanua kwamba, kwa sasa Zanzibar inatarajia kuimarisha miundombinu yake ya viwanja vya ndege ikiwemo ujenzi wa kiwanja cha Nungwi, kiwanja cha Pemba pamoja na ujenzi wa jengo la abiria nambari nne (Terminal 4) katika uwanja wa ndege kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Waziri Dk. Khalid ameitaka kampuni hiyo kuwasilisha mapendekezo ya kiufundi na kifedha ili Serikali iweze kuyapitia na kuchukua hatua stahiki.
Kwa upande wao kiongozi wa Kampuni ya HASSAN ALLAM kutoka nchini Misri wamesema kampuni yao ina uzoefu mkubwa katika masuala ya ujenzi wa miradi mbali kwani zipo nchi nyingi ambazo kampuni yao imetekeleza miradi hiyo.
Aidha, wameeleza watatenga muda maalum kwa ajili ya kufanya ziara maalum katika maeneo yanayokusudiwa kutekeleza miradi ili kujionea na kujirizisha kwa kiasi gani wataweza kuwasilisha mapendekezo yao kwa Serikali.
0 Comments