Header Ads Widget

SUMA JKT YAAGIZWA KUMALIZA JENGO LA HALMASHARI YA WILAYA BUKOBA KWA WAKATI.




NA TITUS MWOMBEKI, MATUKIO DAIMA APP KAGERA.

Mwenyekiti wa Kamati ya siasa ya halmashauri  kuu ya CCM Mkoa wa Kagera Nazir Karamagi aimeigiza SUMA JKT kuhakikisha wanamaliza mradi wa jengo la halmashauri kwa muda unaotakiwa.


Akiongea  katika ukaguzi wa mradi wa jengo la hamashauri ya wilaya Bukoba akiwa katika  ziara maalumu akiambatana kamati ya siasa, Karamagi ameridhishwa na hali ya ujenzi wa jengo hilo kutokana na ubora unaoonekana huku  akimtaka mjenzi kuongeza kasi na nguvu kazi ili kuweza kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Aidha  kamati hiyo imemuomba mkurugenzi kuwapa kipaumbele vijana wanaopatikana kwenye maeneo ambayo serikali itakuwa inatekeleza miradi ili kuendelea kuwa na imaani na serikali yao


Awali akisoma taarifa ya mradi huo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji, Mhandisi Hamza Kambuga amesema kuwa ujenzi umefikia wa  asilimia 80% na umetumia kiasi cha Zaidi ya bilioni 1.8 ambapo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha zaidi shilingi bilioni 2.7.



Kamati hiyo ikiwa halmashauri ya wilaya Bukoba imetembelea pia mradi wa nyumba ya mkurugenzi wa halmashauri ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu milioni 150, jengo la halmashauri, vyumba vya madarasa shule ya sekondari Karamagi sambamba na kuhamasisha upandaji miti ya matunda na kufanya mikutano ya hadhara.


Katika kuadhimisha miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM Kamati ya Siasa ya  halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Kagera inaadhimisha sherehe hizo kwa kukagua miradi mbalimbali ya maenedeleo kwenye wilaya zote za mkoa wa Kagera.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS