Header Ads Widget

SKAUTI MSIBWETEKE KANYAGENI MSIKANYAGWE

 



Na Frederick Siwale - Matukio Daima APP Makambako. 


SKAUTI katika Halmashauri ya Mji Makambako Mkoani Njombe wametakiwa kuwa chachu ya uzalendo na kujituma na " Wasibweteke na kukanyagwa bali wakanyage"                       


Hayo yamesemwa na Mwanzilishi wa Skauti Wilaya na mkoa wa Njombe Kamishna mstaafu wa Skauti Tusiwene Mahenge , wakati wa siku ya maadhimisho ya kumbukizi ya Mwanzilishi wa Skauti  Duniani Sir.Barden Powell.                               



Maadhimisho hayo yamezinduliwa katika shule ya msingi Mwembetogwa " A"  Halmashauri ya Mji Makambako mahali ambapo anafanyakazi Mwl.Diana Nyemele kamishna mstaafu wa Skauti Makambako ikiwa ni sehemu ya kuenzi kazi yake ya kuanzisha na kufundisha Skauti katika mji huo na kisha Wilaya yote ya Njombe.                              



Upande wake Mwl.Diana Nyemele baada ya kupanda mcha wa matunda aina ya Parachichi kati ya miche 10 iliyotolewa na Ofisi ya Halmashauri ya Mji Makambako, alisema Wanafunzi wanatakiwa kuipenda Skauti kwani inafundisha uzalendo, umoja na ukakamavu.     


" Ukijifunza mafunzo ya Skauti huwezi kuwa lege lege na ni lazima utakuwa mzalendo na huwezi kukanyagwa na kuwa mkia bali utakanyaga na kuwa kichwa" Alisema Mwl.Diana Nyemele.                            



Mwl.Nyemele kamishna mstaafu wa Skauti Wilaya ya Njombe ambaye pia ni Mwanachama wa taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza (U.A.K.) Mkoa wa Njombe alipongeza uamuzi wa Skauti Wilaya ya Njombe kutambua mchango wake kwa chama hicho.


Akisoma risala kamishna wa Skauti Halmashauri ya Mji Makambako Lucas Mwinuka alisema chama cha Skauti Ulimwenguni kilianzishwa na Sir.Rord Robert Stephenson Smyth "Baden Powell" februari 22 mwaka 1857 Nchini Uingereza.                        



Risala hiyo ilieleza kuwa Barden Powell alikuwa Luteni Jenerali wa Jeshi la Uingereza aliyeongoza vita katika Nchi mbali mbali likiwepo bara Afrika.                                   


Iliendelea kudai kuwa Baden Powell alijifunza baadhi ya mbinu za kivita kutoka kwa Watoto wa Kiafrika waliolelewa katika mazingira ya porini ambapo mwaka 1907 alianzisha Skauti Nchini Uingereza ,mwaka 1912  alianzisha rasmi Zanzibar (Mkunazini) na Tanganyika ( Magila Tanga )mwa 1917.                                  



Kamisha wa Skauti wilaya ya Njombe Lucas Mwinuka alisema Skauti Wilaya ya Njombe (Mkoa wa Iringa) ilianzishwa  mwaka 2004 na Makambako mwaka 2007.   



Afisa kilimo kata ya mwembetogwa Happy Chambile aliutaka uongozi wa shule hiyo kutunza mche huo wa Mparachichi pamoja na miche mingine iliyotolewa ili kutunza kumbukumbu  ya Skauti Makambako ilipoasisiwa na pia kutunza afya na lishe kwa Wanafunzi katika shule hiyo.



Aidha Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwembetogwa "A" Edina Mahenge alipongeza Uongozi wa Skauti  Kamishna wa Njombe 3Anitha Ngole, Kamishna wa Wilaya ya Njombe Emmanuel Lugongo na Kamishna wa Halmashauri ya Mji Makambako Lucas Mwinuka kwa kutoa heshima ya maadhimisho kuzinduliwa mahali ilipoasisiwa Skauti na kwamba kitaifa yatafanyika Mkoani Tanga februari 2023 .     






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI